Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt John Magufuli ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano anayemaliza muhula wake wa kwanza amesema hakuzaliwa Rais.
Amesema Urais amepewa na wananchi ambao amesema kwa nguvu zao wameweza kufanikisha kukamilika miradi mbalimbali ya kitaifa na iliyofanyika Kilimanjaro.
Aidha amewaomba radhi kwa watu wa Mwanga, Same na Korogwe kutokana na kutokamilika kwa mradi wa maji unaohusisha Mwanga, Same na Korogwe ambao ilibidi uwe umekamilika mwaka 2017.
Kutokana na kuchelewesha kwa mradi huo, Magufuli ameahidi kusimamia mradi huo yeye mwenyewe. Kwa kuwa amesema alikuwa Waziri wa Ujenzi hivyo anajua kuwashughulisha makandarasi.