Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Mimi sikuzaliwa Rais, Urais mlinipa ninyi

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Mimi sikuzaliwa Rais, Urais mlinipa ninyi

Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt John Magufuli ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano anayemaliza muhula wake wa kwanza amesema hakuzaliwa Rais.

Amesema Urais amepewa na wananchi ambao amesema kwa nguvu zao wameweza kufanikisha kukamilika miradi mbalimbali ya kitaifa na iliyofanyika Kilimanjaro.

Aidha amewaomba radhi kwa watu wa Mwanga, Same na Korogwe kutokana na kutokamilika kwa mradi wa maji unaohusisha Mwanga, Same na Korogwe ambao ilibidi uwe umekamilika mwaka 2017.

Kutokana na kuchelewesha kwa mradi huo, Magufuli ameahidi kusimamia mradi huo yeye mwenyewe. Kwa kuwa amesema alikuwa Waziri wa Ujenzi hivyo anajua kuwashughulisha makandarasi.
Kosa kubwa lililofanywa na Watanzania ni kumruhusu Magufuli awe Rais
 
Sidhani kama uraisi alipewa na watanzania
 
Kwa kuwa yeye "hakuzaliwa Rais" atambue kwamba wananchi hao hao waliompa ndio watakaomnyima.
 
Aliingia kwa kura atatoka kwa kura
Na tunamuomba kama tarehe 28/10/2020 kura zake hazitatosha aheshimu maamuzi ya wananchi na amuachie Mh. Tundu SAntiphas Lissu, hatutaki king'ang'anizi wala figisu figisu.
 
Sawa kabisa, Vivyo hivyo tulivyompa yeyey ndivyo tarehe 28.10.2020 tutampa Lissu!
 
Back
Top Bottom