Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli mrudishe January Makamba na Nape wajibu hoja, Polepole anakihujumu chama

Yawezekana kana Pole Pole anaongea ukweli,lakini ukweli huo haujazingatia muda,wakati na hali ya watanzania.

Nikiwa mwanafunzi wa sekondari kipindi hicho nakumbuka kauli ya Mkuu wa Shule alisema"Wanafunzi hawa wakiwa na njaa nikama wanyama,ubinadamu wote huwatoka,husahau kila fadhila wanayotendewa na walimu wao wawapo hapa shule"
Hii ina maana gani?

1: Polepole asidhani kuwa watu hawajui Rais katenda makubwa.Wanaelewa fika ila wanahitaji Rais abalance kidogo miundo mbinu ,ajira kidogo,mishahara kidogo,pembejeo kidogo,nk

2: Watanzania wanahitaji uhuru wao, maono yao, itikadi zao kuheshimiwa ,mfano, jambo dogo tu la kuengua wagombea wa upinzani huku wa chama tawala wakiachwa kinachochea hasara kwa raia nakuona kama serikali inaingilia uhuru wa wananchi kuchagua MTU wameendeleza

3:Kauli za kejeli na vijembe kwa wakati huu zinanasibishwa na chama au serikali Jambo ambalo muda mwingine siyo sahihi ni Mtazamo tu wa Polepole mwenyewe

4😛ole Pole anatakiwa kuueleza umma nini wanakusudia kufanya kwa miaka 5 ijayo kuliko kupoteza muda kumnanga mgombea wa upinzani

5: Watu wanataka kujua ni ahueni gani watapata miaka 5 ijayo tofauti na 5 iliyopita

6: Aelewe kuwa watu wamekata tamaa, hivyo kazi yake kuwa mfariji wa kuueleza Sera nzuri ambazo zinawagusa wananchi hasa waliokata tamaa

7: Jambo lolote lenye mlengo wa kushambulia wapinzani linachukuliwa kama ni mkakati wa serikali kuwahujumu wapiga Kura

8: Aangalie MTU mahsusi wa kujibu hoja za upinzani kwa Uthabiti na kwa ufafanuzi mzuri,watanzania ni waelewa sana wanajua kupima ukweli na propaganda

9: CCM ni chama kikongwe sana, kila MTU anatarajia majibu stahiki na yenye kutia moyo kwani kinachukuliwa kama serikali yenyewe, propaganda zinachukuliwa kama madai ya upinzani ni kweli.

10: Polepole kuleta propaganda kwenye press katika kipindi hiki inaweza kuchukuliwa kama ni hujuma kwa Rais, kumbuka huu ni muda wa kuomba ridhaa kwa wananchi, kila Jambo linatakiwa kuonekana kuratibiwa kitaalam siyo blablaa. Mzee Lukuvi kajibu vizuri sana juu ya maswala ya ARDHI ambayo wapinzani walilalamika, ule ni mfano mzuri wa kujibu hoja kwa kipindi hiki.
 
Mimi niliwapa ushauri was bure CCM waitishe wote waliomshauri m.kiti vibaya wanitokeze kwa hiari yao wentewe na wasisubiri kutafutwa.kwani wameleta wakati mgumu kwa chama kiasi kisicho elezeka.
 
Mikutano ya polepole na waandishi wa HABARI hajaiwahi kunivutia hata siku moja nape nauye alikua fundi Sana wa kuongea na wanahabari hasa nyakati kama hizi.
 
Polepole ni tunu ya taifa, anaweza kuingia kwenye vitabu vya historia kama mwanasiasa mahiri aliyechangia mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini Tanzania, mwacheni afanye kazi yake

Ironically
 
Polepole ni tunu ya taifa, anaweza kuingia kwenye vitabu vya historia kama mwanasiasa mahiri aliyechangia mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini Tanzania, mwacheni afanye kazi yake

Ironically
 

Nimeupenda mchanganuo wako! Ukweli ni kwamba, Polepole na Bashiru ni wasaliti wa harakati zetu kupata tena ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika kipindi kingine cha miaka 5. Time will tell!

Mzee Kinana uko wapi!? Bashiru na Polepole wamekalia kufanya propaganda za kishamba badala ya kuitafsiri na kuieleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa wananchi katika mazingira yao. Hii ni hujuma!
 
Ni wakati wa Rais Magufuli umuulize polepole kwa kipindi chake amefanya kitu gani kwa chama,kwanini wananchi wanaunga mkono upinzani wakati alituaminisha upinzani umekufa?
Waliokufa ni CCM kindakindaki.
 
Wameshachanganyikiwa hao, wanajidai kupuuzia uungwaji mkono mkubwa anaoupata Lissu huko nikoani, lakini kauli zao sasa zimeanza kuwasuta, kumbe sindano za Lissu zinawaingia, naskia na Tume nao wameamua kuwasaidia kina Polepole wanamuita Lissu ajieleze, nawakumbusha Tume Lissu akitoka wamuite na Magufuli aseme kwanini anatumia kofia yake ya Urais wakati huu wa kampeni anavunja sheria makusudi?
 

Sijawahi kumpa usikivu H Pole pole, kwa kuwa nafsi yangu ilimkataa tokea mwanzo.

Alichokutana nacho pole pole ni kubebwa na siasa za kibabe za mwenyekiti na kusahau kabisa siasa za hoja na mantiki.

Sasa kinachodhihirika kwa sasa kwenye ulimwengu wa siasa za bongo ni "Yeye" kuja na nondo za kihoja na kimantiki ambazo kwa pole pole ni kitendawili.

CCM mmelikoroga na hamna budi kulinywa
 
Wamuongeze na Mwanry. Kinyume na hivyo hata 25% ya kura zote Ccm hawapati. Polepole na Bashiru ni wapinzani tangu zamani.
 
Polepole anashindwa katika maeneo mawili tu:-

1. Polepole ni Mwanaharakati sio mwanasiasa. Cheo alichonacho kinahitaji kuwa mwanasiasa na sio mwanaharakati. Kwa sasa CCM haihitaji mtu wa kutoa takwimu na kujibu hotuba za upinzani. Anahitajika mtu anayeweza kuwaambia watu kwa nini wachague CCM huku wakikukumbuka miaka 10 ya Kikwete na ahadi ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania na miaka 5 ya Magufuli na kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda. Je, CCM imefanikiwa kuwapa Watanzania maisha bora?!

2. Polepole anatumia muda mwingi kueleza kile CCM ilichofanya kwa miaka 5 bila kueleza kuwa ni CCM hiyo hiyo ikiwa mtoto wa TANU na Afro Shiraz imekuwa madarakani kwa miaka 43. Je, miaka yote hiyo bado imeshindwa kuondoa changamoto ndogondogo za afya, upatikanaji wa maji safi na shule bora.

Kwa nini iendelee kupewa miaka mingine zaidi?
 
Ingependeza mkatoa hoja zake Polepole ambazo mnaamini zinakihujumu CCM.

Hoja za Polepole haziwezi kujibiwa na Lissu, kiongozi yeyote CHADEMA, sembuse wafuasi wao humu JF. Na huu ni mwanzo tu wa hoja nzito zitakazowatoa wagombea wa CHADEMA ulingo wa kampeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…