Yawezekana kana Pole Pole anaongea ukweli,lakini ukweli huo haujazingatia muda,wakati na hali ya watanzania.
Nikiwa mwanafunzi wa sekondari kipindi hicho nakumbuka kauli ya Mkuu wa Shule alisema"Wanafunzi hawa wakiwa na njaa nikama wanyama,ubinadamu wote huwatoka,husahau kila fadhila wanayotendewa na walimu wao wawapo hapa shule"
Hii ina maana gani?
1: Polepole asidhani kuwa watu hawajui Rais katenda makubwa.Wanaelewa fika ila wanahitaji Rais abalance kidogo miundo mbinu ,ajira kidogo,mishahara kidogo,pembejeo kidogo,nk
2: Watanzania wanahitaji uhuru wao, maono yao, itikadi zao kuheshimiwa ,mfano, jambo dogo tu la kuengua wagombea wa upinzani huku wa chama tawala wakiachwa kinachochea hasara kwa raia nakuona kama serikali inaingilia uhuru wa wananchi kuchagua MTU wameendeleza
3:Kauli za kejeli na vijembe kwa wakati huu zinanasibishwa na chama au serikali Jambo ambalo muda mwingine siyo sahihi ni Mtazamo tu wa Polepole mwenyewe
4😛ole Pole anatakiwa kuueleza umma nini wanakusudia kufanya kwa miaka 5 ijayo kuliko kupoteza muda kumnanga mgombea wa upinzani
5: Watu wanataka kujua ni ahueni gani watapata miaka 5 ijayo tofauti na 5 iliyopita
6: Aelewe kuwa watu wamekata tamaa, hivyo kazi yake kuwa mfariji wa kuueleza Sera nzuri ambazo zinawagusa wananchi hasa waliokata tamaa
7: Jambo lolote lenye mlengo wa kushambulia wapinzani linachukuliwa kama ni mkakati wa serikali kuwahujumu wapiga Kura
8: Aangalie MTU mahsusi wa kujibu hoja za upinzani kwa Uthabiti na kwa ufafanuzi mzuri,watanzania ni waelewa sana wanajua kupima ukweli na propaganda
9: CCM ni chama kikongwe sana, kila MTU anatarajia majibu stahiki na yenye kutia moyo kwani kinachukuliwa kama serikali yenyewe, propaganda zinachukuliwa kama madai ya upinzani ni kweli.
10: Polepole kuleta propaganda kwenye press katika kipindi hiki inaweza kuchukuliwa kama ni hujuma kwa Rais, kumbuka huu ni muda wa kuomba ridhaa kwa wananchi, kila Jambo linatakiwa kuonekana kuratibiwa kitaalam siyo blablaa. Mzee Lukuvi kajibu vizuri sana juu ya maswala ya ARDHI ambayo wapinzani walilalamika, ule ni mfano mzuri wa kujibu hoja kwa kipindi hiki.