Dkt. Bashiru: Tumegusia maeneo ya uchaguzi, yeye alitaka kuzungumza na wagombea wetu wa Zanzibar na Muungano lakini nikamueleza nimetumwa mimi kuzumza nae kwa niaba yao kwa sababu wao wana kazi nyingi. Dkt Mwinyi anaendelea na kampeni na wameanza wamechelewa tarehe 12 mwezi wa tisa na Rais Magufuli ratiba yake nae pia ni nzito na ina kazi nyingi za uongozi nchi pamoja na kampeni.
Na nikamueleza ndio maana hakuweza kwenda katika baadhi ya mikoa ikiwemo Pemba, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Lindi Mtwara na Morogoro.
===========
Akitoa taarifa kupitia vyombo vya habari Dr Bashiru katibu mkuu wa CCM ametangaza kua Dr Magufuli hatoweza kufika mikoa ya lindi,Mtwara na Ruvuma.
Sababu alizotoa ni kua mgombea mwenza alishafika huko (Mama Samia Suluhu)
Akimaliza ratiba ya DSM ataelekea Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na kumalizia Dodoma.
Swali ninalojiuliza Dr Magufuli ana mpango gani na mikoa ya kusini?mbona sio kawaida kwa mgombea Urais kutokufika kabisa kanda fulani wakati wa kampeni.
Je, hii ni fursa kwa Tindu Lissu kwenda kuvunja kabisa ngome za CCM mikoa ya kusini ?Kama kumbukumbu ziko sawa Dr Magufuli ziara zake mikoa ya kusini alirudi na uchovu mara ya mwisho alipoenda na pia ni eneo muhimu sana kimkakati kwa sababu kuna ngome za CUF ambazo zimehamia mikononi mwa ACT, tatu Membe anatoka mikoa ya huko na la mwisho ambalo ni muhimu sana Kuna suala la siasa ya zao la korosho bila kusahau gesi ambayo wananchi walipigwa ipasavyo miaka ya 2012 huko.
Ni mimi mpenda haki, Uhuru na maendeleo, nikiripoti kutoka kichakani.