Zanzibar 2020 Dkt. Magufuli: Nitapata tabu ya kumpata Waziri wa Ulinzi nikichaguliwa kuwa Rais

Zanzibar 2020 Dkt. Magufuli: Nitapata tabu ya kumpata Waziri wa Ulinzi nikichaguliwa kuwa Rais

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema Waziri wa Ulinzi anauwezo mkubwa hata wa kupindua nchi kwa kuwa vifaa vyote viko chini yake

Aidha amemsifu Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye ni mgombea urais Zanzibar kuwa alikuwa waziri wa Ulinzi kwa miaka 11 na hakuwa na tamaa ya kutaka kupindua nchi

Kutokana na sifa hizo amesema atapata wakati mgumu kumpata Waziri wa Ulinzi mwenye kaliba ya Dkt. Hussein Mwinyi kwa muhula wa 2020-2025

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar
 
Kwa kweli kauli Kama hii haikupaswa kutolewa na Rais Magufuli. Kumbe hajiamini na huwa anawaza kupinduliwa? Kisaikolojia maadui zake washamsoma na kujua kuwa Mzee kumbe yupo tayari kisaikolojia kupinduliwa.

Hizi kauli zinawakilisha mawazo ya muhusika...
Hapo upo wasiwasi, kutojiamni na kuhofia maadui...
 
Back
Top Bottom