Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli ongea na wazee, wakuu wa Taifa! Sioni mwisho mwema kama nabii

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Mh Rais, pole kwa mihangaiko ya kupiga kampeni ila nina neno moja juu yako usiku Waleo nalo ni siri japo sio Siri baada yakuandika hapa.

Hali inayoendelea hata tukiwa wanafiki na kuwa tumekunywa maji ya bendera mwisho pumzi zitakata na zikikata mashambulizi yatakuwa makali zaidi kuliko wakati huu tuna nguvu.

Asikudanganye mtu, hali sio hali, yani hata kama ni kwa goli la mkono, ila mtiti huu utakusumbua katk awamu yako ya pili kiasi utahisi kila mtu ni msaliti.

Kuna hali sio ya kawaida huku uraiani, yani watu wamejawa na machungu kiasi hawana pa kupumulia ila tu 28.10.2020.

Majeshi na idara za usalama hawatoweza kudhibiti hili vuguvugu na wakiweza basi watu wengi watakuwa silence jambo litazidi kuibuwa vuguvugu jingine baya zaidi, jambo litazigawa idara zako za ushauri.

Uongozi ni kuacha alama na ili ufanikiwe kubali yaishe, kaa na waliokuweka vua urais wako omba ushauri Ila kumbuka shida ipo nyingine Nani wakukupa honest feedback kwa aina ya uongoz wako mkali sana Mzee wangu hapa tafuta MTU tu akusaidie upewe honest feed back japo sijui kama utaipata Mungu akusaidie.

Pamoja umefanya yote mazuri Ila trust me umeshindwa ishi mioyoni mwa Watanzania. Embu jiulize why? Umeme umetadanza kama uyoga, maji kama yote, mahospitali kama yote, madege, reli.

Yani hakuna mahali hujagusa, umefanya mambo makubwa sana ila umeshindwa kula na kipofu, sasa kipofu kapata kipofu aliewahi kuona hapo zamani Ila baadae akawa kipofu. Amewaambia vipofu wenzake huko sio, hiyo njia sio, wamemwamini ani ni shida ukiweka Jiwe na Magi watu wanapigia Kura Jiwe. Why umesahau wakolon walitupa shanga Sisi tukawapa madini?

Ona sasa mziki huu jamaa Hana bango Hana vyombo vya habari Ila ameteka nchi kweupe.

Waite wazee wakushauri maana najuwa uchaguzi huu hautokuwa Rahisi kama tunavyodhani.

Update
Mkuu ameongea nao nadhani nyote mwajuwa. Ktk vipindi tofauti amezungumza na wastaafu. Na mambo ni poa. Asante
 
Mengi uliyoandika nakubali ila nilipofika pale uliposema kila kitu kagusa, wakati hajaongeza mishahara na stahiki za kisheria za mfanyakazi nikaona sasa wewe pamoja na mada nzuri uliyoileta unapiga propaganda!

Ukatili wa Kuvunja nyumba za wanyonge wakati kuna zuio la mahakama utamuandamana siku zote mpaka anaingia kaburini!
 
Haya mlitakiwa kumshauri toka 2016.

Hali ilivyo asidhani vyombo vya polisi na usalama vitamuokoa. Itafika kipindi hata hao wanaompa kibri watajitoa. Watagawanyika maana ukweli uko wazi

Kweli Rais ili ajaze wafuasi mpaka awasombe kwa mabasi?? Kwamba Wananchi hawawezi kuja wenyewe? Yaani mpaka walipwe? Kwanini wanaanchi wamekuwa na hasira dhidi yake kiasi hiki?

Wakati CCM inalipa na kubeba wahudhuriaji Tundu lisu wahudhuriaji ndio wanaomchangia pesa.
 
Utakavyoona
Lakino hakuna Cha kumtisha Magufuli
Nyie ndio mnadanganyana huko barabarani
Kwani tar 28 mbali
hakuna haja ya kubishana matokeo tutayaona
 
Utakavyoona
Lakino hakuna Cha kumtisha Magufuli
Nyie ndio mnadanganyana huko barabarani
Kwani tar 28 mbali
hakuna haja ya kubishana matokeo tutayaona
Wewe bwana usijifanye unajua kulikoTumainEl hapa jfs tunawajua kila.mtu kwa sifa na tabia zake. Tumain El ni mfia chama wa muda mrefu na mzoefu. Kuna wakati alituhumiwa kuwa yeye ni miongoni mwa Wasiojulikana.

Wewe bwabwaja tu. Leo kapiga magoti kesho atavua shati
 
Madame ndio umecopy uzi wote?? Edit bwana kwa kucopy upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…