Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli ongea na wazee, wakuu wa Taifa! Sioni mwisho mwema kama nabii

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli ongea na wazee, wakuu wa Taifa! Sioni mwisho mwema kama nabii

To be honest Magufuli ana roho ya kukataliwa! Hata hulka zake huonesha ana athari za kukataliwa zinamsumbua sana!

This time wingu sio zuri kwa CCM!

mwenzako anadekiwa lami, uyu mwingine sjui ana bahati gan ya kukoswa na mawe na wananchi
 
Huko Mbarali polisi wameshusha bendera za CHADEMA ili Meko asizione atakapokua anapita kuelekea Mbeya.

Yaani wanamdanganya kwamba anapendwa Tanzania nzima na raia wote wanamkubali.

Atakaposhtuka Lissu atakuwa yuko kwenye kiti cha enzi pale Chamwino.

kiti gan unchoongelea? kile cha ufipa mmeshindwa kununua mnakodisha hadi viti
 
Mh Rais, pole kwa mihangaiko ya kupiga kampeni ila nina neno moja juu yako usiku Waleo nalo ni siri japo sio Siri baada yakuandika hapa.

Hali inayoendelea hata tukiwa wanafiki na kuwa tumekunywa maji ya bendera mwisho pumzi zitakata na zikikata mashambulizi yatakuwa makali zaidi kuliko wakati huu tuna nguvu.

Asikudanganye mtu, hali sio hali, yani hata kama ni kwa goli la mkono, ila mtiti huu utakusumbua katk awamu yako ya pili kiasi utahisi kila mtu ni msaliti.

Kuna hali sio ya kawaida huku uraiani, yani watu wamejawa na machungu kiasi hawana pa kupumulia ila tu 28.10.2020.

Majeshi na idara za usalama hawatoweza kudhibiti hili vuguvugu na wakiweza basi watu wengi watakuwa silence jambo litazidi kuibuwa vuguvugu jingine baya zaidi, jambo litazigawa idara zako za ushauri.

Uongozi ni kuacha alama na ili ufanikiwe kubali yaishe, kaa na waliokuweka vua urais wako omba ushauri Ila kumbuka shida ipo nyingine Nani wakukupa honest feedback kwa aina ya uongoz wako mkali sana Mzee wangu hapa tafuta MTU tu akusaidie upewe honest feed back japo sijui kama utaipata Mungu akusaidie.

Pamoja umefanya yote mazuri Ila trust me umeshindwa ishi mioyoni mwa Watanzania. Embu jiulize why? Umeme umetadanza kama uyoga, maji kama yote, mahospitali kama yote, madege, reli.

Yani hakuna mahali hujagusa, umefanya mambo makubwa sana ila umeshindwa kula na kipofu, sasa kipofu kapata kipofu aliewahi kuona hapo zamani Ila baadae akawa kipofu. Amewaambia vipofu wenzake huko sio, hiyo njia sio, wamemwamini ani ni shida ukiweka Jiwe na Magi watu wanapigia Kura Jiwe. Why umesahau wakolon walitupa shanga Sisi tukawapa madini?

Ona sasa mziki huu jamaa Hana bango Hana vyombo vya habari Ila ameteka nchi kweupe.

Waite wazee wakushauri maana najuwa uchaguzi huu hautokuwa Rahisi kama tunavyodhani.
Alipoingia madarakani alisema waziri kuwa yeye ni dereva hivyo hawezi kumsikiliza mtu, hakuna aliyemsaidia kuchukua fomu ya kugombea urais hivyo hana sababu ya kukusikiliza.
 
Hiyo ndiyo Hali halisi. Kama JPM atashinda 🥺😤 na akaendela na Siasa zake hizihizi....2025 hakutakuwa na CCM

Economy must take a different twist. TRA should not be working on closing down businesses by forcing to collect taxes that do not exist.
Hela zirudi tena kwenye circulation kwa wale wanafanya kazi za halali.
Over and above, we have to change the tone and allow mining and gas/oil investors to start pumping the highly valued and needed cash.
 
The whole truth. TumainEl nini kinakufanya umkatie tamaa Jpm ikiwa ana Tume, Jeshi, MaDED wote wake. Nini hasa kinakufanya uone kama atafeli??
JPM hatafeli. Katiba ya sasa inamlinda mno kuliko chochote kingine. Na CCM itaendelea kuongoza kama katiba itabaki ilivyo

Mtazamo wangu ni kuwa approach ya mambo ya kiuchumi lazima ibadilike. Wafanyabiashara wa ndani wathaminiwe na kusaidiwa. Kuua biashara za ndani ni suicide mission.

Hakuna kiongozi atakayeweza kuongoza watu wenye njaa. Mambo lazima yabadilike ili tuweze kuendelea kuwa na ustawi
 
JPM hatafeli. Katiba ya sasa inamlinda mno kuliko chochote kingine. Na CCM itaendelea kuongoza kama katiba itabaki ilivyo

Mtazamo wangu ni kuwa approach ya mambo ya kiuchumi lazima ibadilike. Wafanyabiashara wa ndani wathaminiwe na kusaidiwa. Kuua biashara za ndani ni suicide mission.

Hakuna kiongozi atakayeweza kuongoza watu wenye njaa. Mambo lazima yabadilike ili tuweze kuendelea kuwa na ustawi
Sawa. Bado huna imani tu!
 
Pambana kuokoa jahazi Mr hali mbaya.


JPM alidhani maflyover, mareli, ma-ndege ndio vitu vya kuombea kura. Kwa dunia ya leo hivyo vitu sio vya kutishia watu; hata watoto wanaviona kila siku kwenye Tv,simu,games nk
Watu wanataka furaha, amani, haki, heshima, shibe - kuishi bila hofu... wameyakosa haya kwa miaka mi5.
Kweli kazi ipo, yaani unasema flyover, ndege na reli umevizoea kwa kuviona kwenye video? Siriazi kabisa? Unasema sio vya kutishia watu, ukienda nchi kama marekani ndege kwa siku zinapaa zaidi ya 200 ndani marekani peke ake achia mbali zinazoenda nje ya Marekani. Ukimsikiliza Tundu ukamuelewa lazima una hitilafu mahali kwa sababu mambo anayohimiza na ahadi zake hazitekelezeki hata kidogo. Huwezi zuia ukusanyaji wa kodi, anavyoahidi ataondoa utitiri wa kodi sio kweli kwani hizo kodi zilikuwepo hata kabla ya Magufuli sema tu hakukuwa na ufatiliaji zikawa hazilipwi ikafikia hatua watu wakaona kama hazipo. Mataifa kama Marekani na wengine msingi wao mkubwa ni kodi na ndio maana walipoona Magufuli anakazia kodi wakastuka waafrika wanaamka. Kitu kingine unachotakiwa kujua hata kama Magufuli ataondoka madarakani ni ngumu kutoa ajira kwa watu wote bila kuwa na mkakati wa mazingira ya kazi. Leo uajiti watu kwa kuwa tu unafurahisha kuwa umetoa ajira mwisho wa siku ushindwe kuwalipa.
 
Back
Top Bottom