Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Sumaye alihamia Upinzani kwasababu alivamiwa na mapepo

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Sumaye alihamia Upinzani kwasababu alivamiwa na mapepo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Magufuli amesema kitendo cha Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Fredrick Tluway Sumaye na Mbunge mteule wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul kuondoka CCM na kuhamia upinzani ni sawa na kushikwa na mapepo lakini sasa roho mtakatifu amewashukia na kurudi CCM.

Amefananisha kitendo hicho cha Sumaye kuhama CCM na kujiunga na upinzani ni sawa na tukio la Malaika waliomuasi Mungu na kutupwa duniani.

Dkt Magufuli ameyasema hayo mjini Babati Mkoani Manyara kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Kwaraa.

Amesema Sumaye ni mwana CCM halisi aliyepotea kwa bahati mbaya kutokana na mapepo yaliyomkumba siku za nyuma pamoja na Mgombea Ubunge Jimbo la Babati Mjini, Paulina Gekul ambaye awali alikuwa CHADEMA.

Amesema Waziri mkuu huyo mstaafu alijifunza mapema akawakimbia na sasa amerudi CCM kwani kiongozi mwadilifuna hicho chama hakikumfaa, kwani kinasimama hadharani na kumtukana kila mmoja na hakina staha.

“Ninamshukuru roho mtakatifu aliyekugusa Mzee Sumaye na ukarudi nyumbani, kufanya kosa siyo kosa, kosa ni kurudia kosaa na ninatambua umefika nyumbani hongera Mungu akubariki na uzao wako.

Hata hivyo, amesema pamoja na kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi, urais ni kazi yenye mateso makubwa.

Amewaomba Watanzania wamchague tena Oktoba 28 ili amalizie kazi alizozianza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Amesema baada ya hapo watachagua wengine ingawa ana uhakika atakuwa wa CCM kwa kuwa mazingira wameweka vizuri na wamejitahidi kuhakikisha nchi inasonga mbele.

Hata hivyo, amesisitiza umoja na mshikamano kuendelea kutawala nchini ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na wasikubali kugawanywa na watu wasio na nia njema.
 
Na mashamba yake pia yalipata mapepo ndio maana akarudi nyumbani kuungana na mashetani, ili mali alizo iba kwa miaka zaidi ya kumi mapepo yazilinde ..

Kuna Marais wanafiki dunia hii ajabu.
Kwani akinyamaza tu kimya na kunadi sera atapungukiwa na nini au hiyo nayo ni sera ndo maana anasema mi5 tena ?.
 
Ni kweli Chadema kuna mapepo, bora amewakimbia
 
Kumtaja taja roho mtakatifu kila eneo, ni dalili ya kua na mapepo!!
 
mzee wa ropo ropo ktk ubora wake...huwa anatamani sana kuwa mchekeshaji tatizo ucheshi haumpendi anaishia kuwa kituko!!.
 
"Hata Geku naye alishikwa na pepo kama la Sumaye. Hivi ni Geku ama Gekulu??" Aliuliza mhe Magufuli.

Kisha akaendelea kwa kusema Gekulu Ni mwanamama mzuri kweli. Kule kwetu mahari yake isinhepungua ng'ombe 70 au 80.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Baada ya kunyang'anywa mashamba, mapepo yakatoka [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Kwa hiyo wakina Askofu Malasusa ndio mapepo?
 
Ni hatari kuwa na viongozi wenye mapepo
 
Back
Top Bottom