Dkt. Makakala nakupa mrejesho kwamba, matumizi ya Madaftari kuhudumia wageni mipakani Karne hii nikufeli kwa wanaokusaidia. Fungeni mifumo mipakani

Dkt. Makakala nakupa mrejesho kwamba, matumizi ya Madaftari kuhudumia wageni mipakani Karne hii nikufeli kwa wanaokusaidia. Fungeni mifumo mipakani

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Last time nilisema Tarakea na Manyovu wanatumia Madaftari kutoa huduma za kuingia na kutoka nchini nikashauri wafanye marekebisho vituo hivi vifanye kazi kama vituo vingine kuleta hadhi Kwa wanaovuka mpaka.

Naomba kumkumbusha Dkt. Makakala kwamba bado Hali hii ipo vile vile pamoja na ushauri niliotoa. Namkubali Sana huyu kiongozi Kwa Sababu amefanya reforms kubwa Sana za huduma Uhamiaji. Most of services sasa unapata online tofauti na huko nyuma. Amefanya KAZI katika speed ambayo inaendana kabisa na elimu yake.

Pamoja na kwamba amefanya vizuri naamini kama amefunga mifumo mizuri Namanga na vituo vingine bado wapo watu wanamkwamisha kufunga mifumo kwenye mipaka mingine. Nachukua fursa hii kumkumbusha asisite kuchukua hatua kwa wanaomkwamisha. Nchi hii isipowekewa mifumo wizi utafanyika Sana

Lakini siyo yeye tu nilitegemea ripoti ya CAG umulike vituo vya mipakani ambavyo hakuna mifumo waje watuambie udhibiti wa mapato na watu unaendaje? Sijaona hii hoja kwenye ripoti Ila namwomba CAG kama ambavyo amekuwa akipata maeneo yakufanya ukaguzi maalumu kupitia vyanzo mbalimbali basi afanye ukaguzi maalumu Kwa TRA na Uhamiaji katika mipaka aone kama mifumo iliyopo inachangiaje upotevu wa mapato.

Ukipita na mgeni akahudumiwa nje ya mifumo wanavyolalamika nakutuona hopeless tunatamani hata serikali ituruhusu diaspora tuwaletee computer mzifunge kwenye mipaka kama tatizo ni vifaa.

Dkt. Please push this agenda kusupot royal tour, wageni wanaokwenda kuangalia kimondo Mbeya wakitaka kwenda Malawi au Mozambique basi wahudumiwe kama wanavyohumiwa wakitaka kwenda Kenya.

Jitahidi kutembelea maafisa wako waliopo kwetu Rukwa mipakani au Kigoma Kwa wakwe zangu uone wanatoa vipi huduma, tunakutegemea Sana Mama Makakala kuikwamua Uhamiaji. Ila tukumbuke pia diaspora, Sisi pia ni Watanzania.

Mwakeye
 
Back
Top Bottom