Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,183
- 2,100
Kufuatia andiko la Mbunge wa Jimbo la Siha na Naibu Waziri wa Afya Godwin Mollel la kuita Kamati ya siasa Wilaya ya Siha kuwa ni vibaraka mtifuano mkali umeibuka na baadhi ya viongozi wakilaani vikali kauli hiyo huku ikielezwa kuwa mbunge huyo hakuwahi kuhudhuria vikao vyovyote vya kamati hiyo .
Akizungumzia kuhusu andiko la Dkt. Mollel aliloliweka kwenye mitandi yake ya kijamii, Facebook na X (zamani Twitter), Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Wilfred Mosi amesema alichokiandika ni maoni yake na sio ya chama.
Mosi, amesema chama hicho kinaongozwa na katiba, kanuni na taratibu zake na kwamba sio kila kitu kinachojadiliwa ndani ya kamati kinapelekwa kwenye mitandao.
"Alichoandika Dk. Mollel kwenye mitandao ni maoni yake na sio ya chama, anajua taratibu katiba na kanuni za chama na kukimbilia kwenye mitando sio tiba" amesema Mosi.
Aliongeza kusema kuwa "Hatujamwomba aandike kwenye mitandao, yanayozungumzwa ndani ya kamati yanabaki kwenye kamati sio kupeleka kwenye mitandao."
Akizungumza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Siha, Meijo Laizer amesema alichokifanya mbunge wao ni kuonesha kiburi kwa chama ambacho kimempa dhamana ya kuwa kiongozi na kwamba anapaswa kuwajibishwa.
"Alichoandika mbunge ni kuonesha kiburi kwenye chama na kuonyesha kuwa chama siyo chochote kwake, kutotambua heshima aliyopewa na watu wa Siha na chama kwani hata hiyo nafasi ya unaibu waziri ameipata kwa sababu yeye ni mwana CCM" amesema Laizer
Ameongeza kusema kuwa "Hata yale aliyoandika mimi binafsi kama kiongozi maoni yangu ni kwamba anapaswa kuchukuliwa hatua. Kwa sababu sidhani kama kiongozi mkubwa kama huyo ambaye amepewa heshima ya kuwa mbunge na naibu waziri anaweza kuonesha dharau za kuidharau kamati ya siasa na kudharau dhamana aliyopewa na watu wa Siha kwa maana ya wana-CCM na wananchi wote wa Siha. Huyu anapaswa kuwajibishwa na mamlaka".
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Siha ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi hakijawahi kuwa na vibaraka na ameshangaa kuona mbunge huyo akitoa maandiko yake ya kuwaita vibaraka.
"Ninacho weza kusema, Chama Cha Mapinduzi haikijawahi kuwa na vibaraka na hakiwezi kuwa na kibaraka kwasababu huyo anayeita kamati ya siasa kibaraka akumbuke kuwa hao ndio waliosababisha aitwe Mheshimiwa mbunge na hata kuteuliwa kuwa Naibu Waziri na ukiona mtu mzima anaanza kutukana watu waliosababisha akafika hapo kuna kitu ambacho hakipo sawa kwenye ufahamu wake na hata Nyati akitaka kufa atarusha mateke mengi."
Kupitia ukurasa wake wa Facebook na Instagram Mbunge wa Jimbo la Siha na Naibu Waziri wa Afya Godwin Mollel aliandika andiko lenye kuonesha ukinzani uliopo baina yake na uongozi wa CCM na aliandika;
"Hapa nilikua namwambia boss, wapinzani wangu jimboni nimewanyoosha hadi sasa wamebaki kutumia vibaraka wao waliopo kamati ya siasa kumlazimisha katibu CCM wa wilaya kuandika barua za vitisho na hata hoja kwenye barua yenyewe hamna"
Mara ooh... unasumbua wazee wa chama, wazee wenyewe nimewapokonya milioni 316 walizotaka kupora ushirika wa Siha Kiyeyu, pia sasa wanalipa zaid ya milioni 200 ambazo hazionekani.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Na wengine nimewafurumusha nikiwa na wananchi 700 na madiwani wakiiba ardhi ya siha kuwekeza kitapeli, ambao walitaka kuuza ardhi ya leoni, sisi na madiwani tuliowafukuza mafisadi hawa tumeandikiwa barua ya kamati ya nidhamu.
Kicheko...! Hivi kwa akili ya kawaida anaeitwa polisi ni mwizi au mfukuza mwizi, ilibidi tucheke sanaaaaa...
Kwasababu kinachosikitisha sisi tuliofukuza wezi ndo tunaitwa kwenye kamati ya nidhamu ilhali wazee waliouza ndo wametushitaki kuwa ndo tuna makosa, na kamati hiyo ya siasa inajua fika kua hao wazee ndo wabadhirifu, na wizara ya kilimo inajua p na vyombo vimethibitisha na document zipo
Boss ameniambia Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka rasilimali za wasiha zilindwe kwa gharama yoyote, na ameniambia anakuja siha mwezi wa 5 kuongeza nguvu kwenye ulinzi wa rasilimali za wasiha.
Nimemuomba ruhusa niingie Siha kuanzia ijumaa ili niwanyooshe hadi jumanne nirud bungeni"