Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
CHADEMA ina miaka mingapi toka ianzishwe? Imeanza kupokea hizo ruzuku toka mwaka gani? Tundu Lisu amekuwa mwanachama wa kawaida na kiongozi ndani ya chama toka mwaka gani?Kwa nini ruzuku ya chama inaingia kwenye akaunti ya benki binafsi ya Mbowe? Hili ni swali ambalo wanachama wanahitaji majibu yake," alisema Tundu Lissu leo akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mlimani City.
Lissu alidai kuwa matumizi ya ruzuku ya Chadema yamekosa uwazi, na akahoji ni kwa nini fedha za chama zinazotolewa na serikali hazipiti moja kwa moja kwenye akaunti rasmi ya chama. "Hatuwezi kuendelea kuendesha chama kwa utaratibu usiofuata taratibu za uwajibikaji na uwazi. Wanachama wanahitaji kufahamu kila senti ya ruzuku inatumikaje," aliongeza Lissu.
Alisisitiza kuwa moja ya sababu kubwa zinazomfanya agombee nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema ni kuhakikisha chama kinarejesha misingi ya demokrasia, uwazi, na uwajibikaji. "Hatuwezi kuwa chama kinachopigania uwazi na demokrasia nchini wakati ndani ya chama kuna mambo ya kificho," alisema Lissu, huku akiungwa mkono na baadhi ya wafuasi wake waliokuwa kwenye mkutano huo.
Una uhakika wanachama hawajawahi kuhoji wala kulalamika?CHADEMA ina miaka mingapi toka ianzishwe? Imeanza kupokea hizo ruzuku toka mwaka gani? Tundu Lisu amekuwa mwanachama wa kawaida na kiongozi ndani ya chama toka mwaka gani?
Kama jibu la hayo maswali ni toka zamani (yaani sio mwaka jana au mwaka juzi) basi hata Tundu Lisu ni sehemu ya huo upuuzi unaofanyika
Inakuwaje fedha ya ruzuku inaingizwa kwenye akaunti binafsi ya mtu kwa miaka yote hiyo na wanachama wapo lakini hawahoji wala hawalalamiki?
Ni utaratibu gani huo unaoruhusu fedha za taasisi kuingizwa kwenya akaunti binafsi?
Mtu anayesubiri kuwa mwenyekiti ndio ashughulike na changamoto huyo na yeye pia ni changamoto pia. Yaani usubiri kuwa kiongozi ndio upiganie taasisi yako?
Nachofahamu mimi kiongozi mzuri alitakiwa aonyeshe kwa vitendo kuwa haya si mambo mazuri toka akiwa mwanachama wa kawaida achilia mbali kuwa hadi makamu mwenyekiti.