Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Godwin Mollel amewataka wananchi kutokuogopa maneno yanayoendelea mitandaoni kuhusu chanjo ya Uviko-19 kwani chanjo hiyo ni salama.
Dk Mollel amesema hayo katika mkutano mkuu wa wadau wa huduma za elimu ya afya kwa umma uliofanyika jijini hapa.
Amesema Tanzania ni Taifa la Mungu hivyo hatma yake iko mikononi kwa Mungu huku akiwataka kuchapa kazi na kuwasihi waandishi kuzingatia maudhui yanayofaa kurusha kwenye vyombo vya habari.
"Msiogope yanayoendelea mitandaoni na kwenye vyombo vya habari ni kawaida tu, mambo yatakaa vizuri…Mkachape kazi hayo mengine mtuachie sisi maronaldo wenu wao watakuja na wataondoka wakiwa wamefunga goli 0…Hali ya chanjo inaenda vizuri tunaweza kuwaacha wapumbavu na wajinga tukaenda nao,"amesema.
Katika kutoa elimu kwa umma aliwataka wadau hao kuwashirikisha watu maarufu, wasanii na viongozi wa dini ili kufikisha elimu kwa umma kuhusu umuhimu a chanjo ya Uviko 19 hasa sehemu za vijijini.
Aliwataka wadau kutokujielekeza katika kufanya semina na makongamano na badala yake bajeti iliyowekwa itumike kuwawezesha wadau kuwafikia wananchi ili kutoa elimu ya afya kwa umma na chanjo ya Uviko-19.
Mwananchi