Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haiwezi kuwa.VP Mpango, mtu mnyenyekevu, mcha Mungu, msema kweli na nguli wa uchumi.
I really hope kati ya Mpango au Majaliwa mmoja wao akwee pale juu baada ya mama kumaliza kazi yake.
Mtanzania hutakiwi muonea huruma,W
Watanzania wameathiriwa kisaikolojia. Wamefanywa kuamini kwamba kupambania haki zao ni kuvunja sheria hivyo wamechagua kuwa wapole ili wasivunje sheria.
Otherwise demokrasia ni ya makaratasi tu.
Ndio maana degree zenu siku hzi pia ni za kumeza summary. (Kukariri vi-summary tu bila deep knowledge ya jambo husika)Hilo gazeti loote la kwako, wengine wana summarise
Yaani nimekaa iramba ndugutiMungu wako si mungu wao. Wanachofanya ndio haswa wanatekeleza malengo na matakwa ya mungu wao.
Siku yao haiko mbali sana, wacha waendelee kututesa.
Inatia Hasira sana yani.Mtanzania hutakiwi muonea huruma,
Kama watu wamepiga Bilioni 480 kisa wamechelewesha kulipa wakandarasi wategemea nini?
Hizo pesa zilikuwa zinaweza jenga
Madarasa 24,000, ambayo yangetoa shule 1200
Hapo tumechukulia kila Darasa lijengwe kwa 20Mil, kila shule iwe na Madarasa 20
Hapo hayo Madarasa Mapya yangetosha wanafunzi Milioni 1, kama kila darasa litabeba wanafunzi 45 kama sera ya elimu esamavyo.
Ingejenga Vituo ya Afya 1200, hivi vituo vya Afya vingewekwa 6 kwenye kila wilaya.
Ingejenga Vituo vya Afya 3200, kwamba kila wilaya ingepata vituo 16
Ingejenga nyumba za walimu 16,000
Hizo pesa zingetosha kujenga barabara za lami KM 200-400, maana yake Barabara kutoka Igawa hadi Tunduma ingewezekana kabisa
Sasa angalia hayo yote afu watu wametulia tu hawahoji, wala hawaoni mtu aliyewajibika, waziri wa fedha yupo, wa ujenzi yupo
Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania amesema “Malengo makuu ya dira ya Mwaka 2025, Maisha bora kwa kila Mtanzania, Kudumisha amani, usalama na umoja katika Nchi, Utawala bora, Jamii iliyoelimika vyema na inayojifunza, tano ni uchumi imara na shindani.”
Pamoja na hatua kubwa ambayo Nchi imepiga bado kuna changamoto mbalimbali zilizosababisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2000-2025 kutofikiwa kikamilifu mfano:
“Changamoto ya umasikini wa kipato na lishe duni, kwa mujibu wa utafiti wa Mapato na Kaya, takribani 26.4% ya Watanzania wanaishi chini ya kiwango cha umasikini wa kipato, ambayo ni zaidi ya Robo na Wananchi masikini zaidi wanaishi vijijini 31.3%.
Kuna mikoa, nitataja michache Kagera, Kigoma, Singida, Tabora na Dodoma ambayo kiwango cha umasikini ni kikubwa zaidi kwa sababu mbalimbali kutokana ikiwemo matatizo ya Kihistoria na miundombinu duni.
Aidha, tofauti ya kipato miongoni mwa Watanzania imeendelea kuongezeka licha ya kufanya vizuri katika kigezo cha kufanya vizuri uchumi jumla.
Kiwango cha tofauti ya kipato kwa kutumia kipimo cha uwiano kiliongezeka kutoka 0.34 Mwaka 2011/12 mpaka 0.38 Mwaka 2017/18.
Katika kipindi kama hicho, kipimo hicho cha tofauti ya kipato kwa maeneo ya Mijini nacho kiliongezeka kutoka 0.37 hadi 0.41.
30% ya Watoto chini ya miaka mitano wana udumavu Nchini
Akizungumza katika uzinduzi wa Mchakato wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti wa Mapato na Kaya.
Amesema “Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2022 unaonesha kuwa 30% ya Watoto wenye Umri chini ya miaka mitano wana udumavu na 9% ya Watoto wana udumavu mkali.”
Dkt. Mpango: Elimu yetu haikidhi mahitaji ya soko la ajira
Kwa upande wa kuwa na jamii iliyoelimika na inayojifunza, tumepata mafanikio ya kuridhisha ikiwemo kuongezeka kwa Wanafunzi katika ngazi zote za elimu.
Viwango vya ufaulu vimeongezeka, uwezo wa kusoma na kuandika Nchini unakadiriwa kuwa 92%.
Pamoja na mafanikio hayo bado vijana wengi wanaomaliza masomo hawapati fursa za ajira, pia elimu yetu haikidhi mahitaji ya soko la ajira wala kuwezesha wahitimu kujiajiri.
Jitihada za kurekebisha hali hiyo zinaendelea ikiwemo kupitia sera ya elimu na mitaala.
Ni kweli Kagera ni maskini zaidi ya Pwani na Lindi?Ni jambo jema
Kwa mujibu wa utafiti wa Kipato Cha Kaya Mikoa mingine ni
Kigoma,
Singida,
Dodoma,
Tabora
Kagera.
VP Mpango, mtu mnyenyekevu, mcha Mungu, msema kweli na nguli wa uchumi.
I really hope kati ya Mpango au Majaliwa mmoja wao akwee pale juu baada ya mama kumaliza kazi yake.