Dkt Mpango aipongeza Wizara ya maji kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maji Nchini

Dkt Mpango aipongeza Wizara ya maji kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maji Nchini

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
DKT MPANGO AIPONGEZA WIZARA YA MAJI USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI NCHINI

BAHI-DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdori Mpango Leo Agosti 19, 2024 ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Maji Ibihwa, Wilayani Bahi, Jijini Dodoma.

Mhe. Mpango ameipongeza Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri na utejelezaji wa miradi ya maji nchini.
Pamoja na hilo pongezi hizi zimejukisha mradi wa maji Ibihwa na kusisitiza kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima ili Wananchi wapatie huduma ya Majisafi na kwamba ahadi ya kukamilisha mradi wa Ibihwa ifikapo tarehe 30.09.2024 itekelezwe kwa wakati.

Aidha akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Waziri wa Maji (Mb.), Mhe. Jumaa Hamidu Aweso amewahakikishia Wananchi wa Kijiji cha Ibihwa kuwa, Wizara itakamilisha mradi huo kabla ya tarehe 30/09/2024 na kwamba Maji yatafika pia katika Mji wa Bahi.

Mradi wa Maji Ibihwa unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Milioni 709 na unasimamiwa na Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ukiwa umefikia asilimia 75 ya utekelezaji na umeanza kutoa huduma kwa Wananchi, ambapo mradi huu utawanufaisha wananchi wapatao 8,932 wa Kijiji cha Ibihwa.
 

Attachments

  • IMG-20240819-WA1620.jpg
    IMG-20240819-WA1620.jpg
    233.7 KB · Views: 5
  • IMG-20240819-WA1621.jpg
    IMG-20240819-WA1621.jpg
    252.3 KB · Views: 5
  • IMG-20240819-WA1529.jpg
    IMG-20240819-WA1529.jpg
    212.8 KB · Views: 3
  • IMG-20240819-WA1528.jpg
    IMG-20240819-WA1528.jpg
    207.3 KB · Views: 4
  • IMG-20240819-WA1527.jpg
    IMG-20240819-WA1527.jpg
    149.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom