informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 184
- 170
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Benki Kuu na taasisi za kibenki kuona namna ya kupunguza gharama kwenye huduma za kibenki za kidijiti ili kuwezesha wananchi wengi kutumia njia ambayo inaleta tija mbalimbali ikiwemo kuipunguzia Serikali gharama ya kutengeneza sarafu.
Hayo ameyaeleza leo Machi 28, 2025 katika hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya NMB Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, gharama za kidijiti zinaonekana kuwa kubwa jambo ambalo linaweza kwenda kinyume katika kupunguza matumizi ya fedha taslimu.
"Ni muhimu kuangalia namna bora ya kupunguza gharama za huduma za kibenki za kidijiti ambazo baadhi zinaonekana kuwa kubwa na hivyo kukindhana na lengo la Taifa letu, kupunguza matumizi ya fedha taslimu ili kurahisisha malipo, kuchochea matumizi na kuipunguzia Serikali gharama ya kutengeneza sarafu."amesema Dkt. Philip Mpango
Licha ya kusisitiza umuhimu wa suala hilo, apongeza amepongeza NMB kwa mafanikio wanayoendelea kuonesha katika utoaji wa huduma kupitia njiani mbalimbali hasa za kidijiti ikiwemo utoaji wa mikopo salama yenye riba nafuu.
"NMB ni miongoni mwa mabenki yanayokua kwa kasi kwa kutengeneza faida, gawio la jumla la kila mwaka kwa wana hisa limeongezeka kutoka Tsh. Bilioni 97 mwaka 2021 na mwaka 2023 lilifikia Tsh. Bilioni 181, lakini kwa upande wa Serikali gawio ambalo tulipata liliongezeka kutoka Tsh. Bilioni 30.8 (2021) na lilifikia Tsh. Bilioni 57.4."amesema Dkt. Philip Mpango
Aidha awali wakati akitoa taarifa kwa mgeni rasmi kuhusu hatua mbalimbali ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Benki ya NMB, Afsa Mtendaji Mkuu (CEO), Ruth Zaipuna amesema kuwa wameendelea kuweka mikakati ya kuwafikia wananchi wa vijijini katika kutumia huduma za kibenki.
"Ripoti ya 'FinScope Tanzania 2023' ilionesha kwamba ni asilimia 22 tu ya watanzania ndio wanaotumia huduma za kibenki, ripoti hiyo pia ilionesha kwamba watanzania wengi walio nje ya mfumo wa kibenki ni wale wanaoishi maeneo ya vijijini"amesema Ruth
Ameongeza "Baada ya kutambua hilo, mwaka 2024 Bank ya NMB tulikuja na mpango mkakati wa kupeleka huduma za kibenki vijijini hasa kupitia uwekezaji wa wakala lakini pia kutumia teknolojia."
Amesema kuwa mpango huo unalenga walau kila Kijiji Tanzania kinakuwa na mawakala angalau wawili wa Benki ya NMB kwa lengo la kuwasogezea wananchi huduma za kibenki, ambapo amesema katika mkakati huo kwa mwaka jana (2024 ) walifanikiwa kufikia vijiji takribani 2000 nchini huku wakiwa wameanzisha jukwaa maalumu la 'Kijiji day' ambalo utumika kufikisha elimu na huduma za kibenki kwa Wananchi waliopo vijijini.
Sanjari na mikakati hiyo, ameeleza kwamba Benki ya NMB imetenga zaidi Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya kufanikisha mkakati wa Kitaifa wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia, ambapo amesema kuwa fedha hizo zipo tayari kutolewa kwa wafanyabiashara na wadau wanaotekeleza mkakati huo kupitia utaratibu wa mkopo.
"NMB tunashiriki katika kuhakikisha tunashiriki katika kufanikisha mkakati wa Taifa wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia, tayari tumetenga zaidi ya Bilioni 100 maalumu kabisa kwa ajili ya miradi na biashara zinazopeleka na kusambaza nishati safi ya kupikia kwa watanzania"amesema Ruth
Aidha katika taarifa yake imeeleza kwamba Benki ya NMB katika Mkoa wa Dar es salaam ina jumla ya matawi 34, ikijumuisha matawi mawili yaliyozinduliwa leo ambayo ni tawi la Kinyerezi na Chanika, lakini kwa Nchi mzima inaelezwa kuwa kuna jumla ya matawi 241, Mawakala elfu 50 huku mpango wao katika mwaka huu 2025 ni kufikisha mawakala elfu 70 Nchi nzima, pia taarifa hiyo imeeleza kuwa wana wateja takribani milioni nane.