Dkt. Mpango: Mkandarasi wa Bwawa la Nyerere hana Uzoefu, pia mradi upo nyuma ya muda

Hapa kunajambo tunadanganuwa waz waz mbona huu mradi ulienda kwa spidi wkt wa Magu na kwa nn sasa unakwamwa nakumbuka huu mradinulikuwa uanze zamani lkn wapi hawa watu wanatudanganya waz waz siamini conaractor hajui kaz alifanyaje mradi wakt wa magu uende fasta saiz usimame magu alisema hv wanauzaga majererator biashara yao...
 
Ulikuwa uanze zamani ya lini wakati mwanzoni ilikadiriwa ungeanza May 2022, lakini pakatokea tatizo ambalo lili-delay kazi kwa miezi 5.

Hilo suala la subcontractor, tafuta CAG Report 2019-2020 wamelielezea! And remember, ripoti hii ilikuwa imeangalia ujenzi kwa kipindi cha 2017/2018-2019/2020, na kwa kipindi CAG alikuta kuna Subcontractors 21 and 9 Subconsultants TO ALL MAJOR PROJECT COMPONENTS!

Uzuri ni kwamba, by the time only 36.7% ya kazi ndizo zilikuwa subcontracted huku mkataba ukiruhusu a maximum of 50%. Hata hivyo, CAG bado alikuwa na concern kwa sababu miongoni mwa kazi zilizokuwa subcontracted ndo hizo nilizotaja hapo juu kwamba kulikuwa na Subcontractors 21 and 9 Subconsultants TO ALL MAJOR PROJECT COMPONENTS!
 
Mhh Tanzania safari bado ni ndefu wajameni. Huyu si alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango..sasa kulikoni tena?
 
Crane la tani 26 liko wapi kwani?
Mkuu ni vema tu wahusika waseme wazi tu kuwa wameachana na mradi huo wa bwawa ka Nyerere, tutawaelewa tu maana wana haki na nguvu za kufanya hivo. Hii ya kudanganya danganya wanajipotezea muda tu kama ule uongo wao wa yupo ofisini na lundo la mafaili.
 
Tanzania tuna tatizo la upotoshwaji wa habari, na hii chanzo chake ni ukanjanja wa wanahabari wengi tulionao.

Habari isiyokuwa na ukweli ndio inaibua mjadala miongoni mwa watu na ile yenye ukweli inapita kama vile haina umuhimu wa kujulikana.
 
Tanzania tuna tatizo la upotoshwaji wa habari, na hii chanzo chake ni ukanjanja wa wanahabari wengi tulionao.

Habari isiyokuwa na ukweli ndio inaibua mjadala miongoni mwa watu na ile yenye ukweli inapita kama vile haina umuhimu wa kujulikana.
Mkuu Bukililo,

Kwa hili Waandishi itakuwa unawaonea...

Tafuta Ripoti ya CAG (For Development Project) ya mwaka 2019/2020 na humo utaona the following highlights ambazo nilizitoa kwenye post moja wapo:-

Kutokana na hilo, CAG akaeleza wazi kwamba HII INAWEZA KU-IMPAIR THE QUALITY OF WORK hata kama the quality risks inaangukia kwa Contractor.


3. Contract and Project Design Requirements ilikuwa inataka Contractor ajenge 2 Diversion Tunnels. Kwa mshangao wa CAG, Contractor akajenga ONLY ONE Diversion Tunnel!

Matokeo yake, iliponyesha mvua na mto kujaa, maji yakafanya mambo yake!!

What happened next day? Wakati mnaambiwa mambo ni FIRE kumbe uhalisia project ilikuwa DELAYED FOR 5 MONTHS!!


Na ripoti zingine zinaonesha, hata baada ya hiyo delay inayooneshwa hapo juu, bado delays iliendelea! Kwa mfano, as at December 31, 2020 ONLY 28% of the project was completed out of around 46% lakini huku mitaani watu walikuwa wanaaminishwa mambo ni FIRE!
 

Ufisadi mkubwa sana umefanyika kwenye mradi huu. Sehemu kubwa ya kazi ya ujenzi inafanywa na Sino Hydro. Ukitembelea mradi huu unakuta hawa waarabu wana supervise kazi tu.
 
Taratibu za kumpata mkandarasi zilifuatwa? Kama zilifuatwa ilikuwaje apewe huyu asiye na uzoefu. Huu ni mradi mkubwa sana na unatumia pesa nyingi za watanzania. Ilitakiwa umakini mkubwa katika kumpata mkandarasi. Hii si sawa na kipande cha barabara cha km 2! Wasiwasi wangu ni viwango, isije ikawa kwa kukosa uzoefu isije kutengenezwa bwawa lisilo na viwango sahihi. Madhara yake kila mtu anayajua!
 
Sasa si bora waanze kufuga kambale na perege kwenye hilo shimo? Au kilimo cha nyanya na vitunguu? Si ndiyo uwekezaji? Au?
Tusubiri hadi wazingu wapone corona mpaka lini?
 
Mkandarasi awezi kufanya deviation kubwa from the initial design bila ya makubaliano na mteja kwanza.

Ni sawa na wewe ulipie kuwekewa roof ya vigae kwenye nyumba yako, halafu ukute bati huo ugomvi auwezi kuwa mdogo.

Lakini ukikaa kimya kwenye mabadiliko kama hayo maana yake ni kwamba uliridhia; mkaguzi kabla ya kulaumu alitakiwa akuulize wewe mwenye mradi kama unajua umewekewa bati badala ya vigae.

Most likely hayo mambo yapo kwenye PID ya project kama kuna changes what agreements needs to be made first.

Naanza kupata mashaka na quality ya auditors wa serikali. Mtu anasema nimekuta hivi lakini asemi alimuuliza nani sababu za deviation sio client wala contractor; ila analaumu tu.
 
Mkandarasi awezi kufanya deviation kubwa from the initial design bila ya makubaliano na mteja kwanza.
We jamaa unapenda sana kujitoa ufahamu!! Bila makubaliano kivipi wakati unaona kabisa ripoti inasema:-
This is contrary to Section 12.3 of the Employer’s Requirement Vol II of December, 2017 which requires the contractor to construct two tunnels with a total discharge capacity of 7000 cubic metres per second.
Au huwa husomi?
Ni sawa na wewe ulipie kuwekewa roof ya vigae kwenye nyumba yako, halafu ukute bati huo ugomvi auwezi kuwa mdogo.
Uwe unasoma badala ya kukimbilia ku-comment ili mradi ujaribu kutetea
Naanza kupata mashaka na quality ya auditors wa serikali. Mtu anasema nimekuta hivi lakini asemi alimuuliza nani sababu za deviation sio client wala contractor; ila analaumu tu.
SHAME ON YOU!!

Yaani Contract Requirement inataja 2 Diversion Tunnels lakini inajengwa 1 Tunnel halafu CAG anahoji bila aibu unasema una mashaka na quality of auditors?

Yaani badala ya kuhoji walio-approve single instead of 2 tunnels unahoji uwezo wa aliyefichui huo ujinga ambao ulipelekea poject ku-delay kwa miezi 5?

Yaani nyie ni watu wa ajabu sana!!
 
Tatizo lako unapenda majibu ya sisi na wao badala ya kuangalia facts or even how things work in some instances.

Inawezekana kabisa kulaumu kazi ya CAG nimekosea maana una tabia ya kuleta extracts which justifies your position badala ya link nzima ya source at the bottom ili na wengine wajiridhishe.

Project kubwa kama hiyo inakuwa na kitu kinaitwa Project Initiating Document (PID) inayoelezea scope ya kazi ni sehemu ya mkataba na ndipo ata huyo mkaguzi alipojua nini kilitakiwa kujengwa na kipi kimejengwa.

So to diversify from PID agreement without the consent of the client au yeye mwenye kuagiza ili apunguze gharama hilo swala aliwezekani vinginevyo mkataba unavunjwa na unashitakiwa.

Ndio maana diversion ya kwenye mkataba wa ujenzi kama huo contractor awezi kwenda nje PID bila ya client recommendations au blessing kama walikutana na engineering challenges zingine from the original design. Sasa wewe unataka kuaminisha umma contractor hajui kazi.
 
Lakini kampuni ya pole pole inajitahidi sana kuchimba hilo bwawa, ingawa ni subcontractor tu[emoji23]
 
Unachekesha sana we jamaa

Yaani pamoja na kuambiwa hiyo ni CAG Report for Development Projects 2019/2020 bado unadai uletewe link?! Hivi nini maana ya kutajiwa Title kama sio kutoa fursa ya kila mtu kutafuta ripoti husika aisome kwa mapana na marefu?
Weka hizo facts hapa chini, with REFERENCES!

Btw, yaani bado kabisa unashindwa kuelewa?! Design na Mkataba VYOTE vilitaka TWO Diversion Tunnels.

Contractor akajenga SINGLE TUNNEL

Matokeo yake,
This eventually led to project delay for five months as a result of the coffer dam overtopping and subsequent flooding of the diversion tunnel.
Yaani pamoja na hayo bado unatafuta sababu za ku-justify kilichofanyika licha ya kuona damage ilishatokea?! Ina maana bado huoni kwamba hiyo Client Blessing ndiyo imeleta yote hayo?!

Na hapa nimesema Contractor HAJUI KAZI au nimesema Contractor ali-opt kwenda kinyume na Mkataba ulivyosema?!
 
[emoji106] Hata kwa mtaalamu wa kawaida hili lazima lingetokea tu. Implementation ya project kubwa kama hii kutumia feasibility study iliyofanyika miaka 50 iliyopita haiingii akilini, worse still unateua consultant ambaye ni mtaalamu wa barabara. What do you expect?
 
Tundu lisu kipindi wamesaini tena huyo mkandarasi na akashinda lisu bungeni alisema kwa huko kwao hiyo kampuni niya kutengeneza chemba aliishia kupiga marisasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumeingizwa choo cha kike .RIP Magufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…