Dkt. Mpango: Nusu ya wabunge hawajalipwa mshahara wa mwezi Machi

Dkt. Mpango: Nusu ya wabunge hawajalipwa mshahara wa mwezi Machi

baadhi ya watumishi pia hawakulipwa malimbikizo yao ya mishahara, ambapo waliahidiwa kulipwa mwezi huu na msemaji wa serikali.
hii ni haki yao tafadhali kabla hujala kiapo hiyo kesho wafute machozi watumishi hawa wanao dai haki zao za malimbikizo ya mishahara, kukalia haki za watu ni dhambi kubwa sana,epuka dhambi hiyo ya manunguniko, Mungu atakubariki zaidi.
 
Kuna wabunge wanaishi kama malaika wanaendesha VXR
Kuna wanafunzi wanakaa kwenye mawe kwa kukosa madawati.
Kwa muktadha huu unqdhani hizo 3.9 B ziende wapi kati ya hizo sehemu mbili?
Ziende Kwa wanafunzi bila kupepesa macho
Nalog off
 
wasilipwe kabisa hawana tija yoyote kwa nchi, yaani uache kulipa madaktari & waalimu halafu uende ukawalipe akina Kibajaj na Msukuma...hiyo akili au matope?!
 
kwa maoni yangu ni bora wasilipwe wabunge kisha wakalipa malimbikizo ya mishahara ya watumishi ambayo wamekuwa wakidai kwa kipindi kirefu, hilo ni jasho lao lililo kauka. walipeni haki zao ili Mungu aweke baraka ktk Serikali.
 
Yaani waliwekwa pale ili wawatetee / kuwawakilisha wananchi na wenyewe wanalalamika ?, Bora, warudi tu mtaani hawana maana...

By the way walivyo walafi huenda mshahara haujasoma ila posho n.k. zinasoma maradufu ya mishahara (waache na wenyewe watuwakilishe kwenye huu uchumi wa kati wa kwenye makaratasi ambao hauna uhalisia)
 
Waziri wa fedha Dr Mpango amesema nusu ya wabunge hawajalipwa mshahara wa mwezi March 2021.

Ndugu Mpango amesema amekuwa akifuatilia huku na kule kuhakikisha wabunge wanalipwa.

Kwa sasa Dkt. Mpango ameteuliwa kuwa makamu wa Rais.

Kila zama na kitabu chake

Maendeleo hayana vyama!
BUNGE gani hili hata wasipolipwa ni sawa tu kwani lipo kwa maslahi ya nani.halitusaidii wananchi wala haliwasaidii watumishi wa umma.Ni bunge la wanafiki tu ndo maana linamsifia makamu wa rais as if ndo anaanza kazi leo wakati yuko ndani ya mfumo miaka nenda rudi wala hatukuona lolote.yy alikuwa anasukumwa tu pale na JPM halafu leo aonekane ni mzuri.Na wtz tuache unafiki wa kuwapongeza watu ambao hata hawana ufanisi wowote ndani ya nchi hii.
 
Waziri wa fedha Dr Mpango amesema nusu ya wabunge hawajalipwa mshahara wa mwezi March 2021.

Ndugu Mpango amesema amekuwa akifuatilia huku na kule kuhakikisha wabunge wanalipwa.

Kwa sasa Dkt. Mpango ameteuliwa kuwa makamu wa Rais.

Kila zama na kitabu chake

Maendeleo hayana vyama!
Aende zake huko, anatetea watu ambao hawana kazi kazi kubwa ni kugonga meza na huku wanalipwa kila siku 340,000 badala ya kutetea watu wanao sumbuliwa na TRA, trafic n.k
 
Back
Top Bottom