Dkt. Mpango: Singapore kuboresha Bandari ya Dar es Salaam kwenye Miundombinu na Menejimenti ili iwe ya kisasa barani Afrika!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Makamu wa Rais Dr Mpango amesema ameongea na wataalamu wabobezi wa mambo ya bandari ambao watakuja nchini kuifanyia maboresho makubwa bandari ya Dar es Salaam.

Dr Mpango ambaye alikagua teknolojia za kisasa za bandari zinavyofanya kazi amesema Singapore itaboresha miundombinu na menejimenti ya bandari na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi barani Afrika.

Dr Mpango yuko ziarani nchini Singapore.

Chanzo: TBC
 
Tatizo wanaongea mnooooo. Mambo ya TPA tu hayo, VP ni mtu mkubwa sana.

Ni kweli hilo mkuu. Inaniuma sana Rais kuwa kwenye ufunguzi wa hospital, sijui vifaa tiba nk. Ona huyu nae yuko kwenye mambo ya bandari - sijui mamlaka ya bandari kama haiwezi kuzungumzia uendeshaji.

Tuna viongozi wanaowaza na kushiriki katika mambo madogo madogo sana!!
 
Kama inaweza kuboreshwa ikawa ya kisasa zaidi Afrika, hii ya Bagamoyo ya nini sasa! Na hii ya menejimenti isije ikawa kama wale Net group solutions wa tanesco ya Mkapa.
 
Good!! Mama anafungua nchi!! Yule mshamba alituchelewesha sana!
Hizi hasira zote ni sababu yule mshamba alikuachia mtoto wa kulea?

Kwani ulikuwa unampa tu bila kujali kama kuna kesho?
 
Hata ningekua mwanamke kweli kumpea yule chizi nisingewahi.
 
Ni kweli hilo mkuu. Inaniuma sana Rais kuwa kwenye ufunguzi wa hospital, sijui vifaa tiba nk. Ona huyu nae yuko kwenye mambo ya bandari - sijui mamlaka ya bandari kama haiwezi kuzungumzia uendeshaji.

Tuna viongozi wanaowaza na kushiriki katika mambo madogo madogo sana!!
Hivi kuboresha bandari inayo toa uchumi kwa nchi ni jambo dogo? Tuache chuki zisizo na tija.
 
Singapore, nilikuwa harbour pale. Meli inaingia bandarini kila baada ya dakika tano. Kwa sababu zile zipo kule off shore,ishirini au thelathini,all the time. Kwa hiyo wanasubiri kidogo tu ili wakel(mawimbi) ya meli ya mbele ipungue, halafu wanakwenda.

Likewise angani,a plane landing every five minutes(or less than five minutes). Yote hii inatokea 24-7,kwa bandari na airport.
 
Mhhh! TRC walikuwa na Kampuni iloitwa Management Solution. Hwa walipewa jukumu la kufanya reforms na kubadili muundo wa TRC ili ijiendeshe na Wahindi walipewa jukumu la uendeshaji. Kilichokea kilistaajabisha dunia!
 
Kama inaweza kuboreshwa ikawa ya kisasa zaidi Afrika, hii ya Bagamoyo ya nini sasa! Na hii ya menejimenti isije ikawa kama wale Net group solutions wa tanesco ya Mkapa.
Utapeli wa kisiasa uko kiwango cha juu zaidi katika historia ya nchi hii chief!
 
Singapore wana kampuni yao inaitwa evergreen inafanya vizuri sana kwenye mambo ya shipping ni vizuri waje watupe uzoefu
Kabisa naipata sana hiyo kampuni..

Vipi mkuu wangu bado upo SA?
 
Makamu wa Rais Dr Mpango amesema ameongea na wataalamu wabobezi wa mambo ya bandari ambao watakuja nchini kuifanyia maboresho makubwa bandari ya Dar es Salaam.

Dr Mpango ambaye alikagua teknolojia za kisasa za bandari zinavyofanya kazi amesema Singapore itaboresha miundombinu na menejimenti ya bandari na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi barani Afrika.

Dr Mpango yuko ziarani nchini Singapore.

Chanzo: TBC
Kiko wapi sasa?
 
Weka mkataba hapa we mzee Mpango

mnatuchukulia raia kama mazoba sana
 
Back
Top Bottom