Dkt. Mpango: Viongozi acheni kupiga 'Vistoristori' na Madereva wenu ndani ya Magari ili Siri zenu zisisambazwe

Dkt. Mpango: Viongozi acheni kupiga 'Vistoristori' na Madereva wenu ndani ya Magari ili Siri zenu zisisambazwe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Katika kutunza Siri za Watumishi wa Serikali niwaase sana nyie Wakuu wa Wilaya na Watendaji Wengine Serikalini muache Kupiga Vistorivistori mkiwa na Madereva wenu ndani ya Magari yenu ili kuepuka Siri zenu Kuzagaa na Kuaminika kwao hawa Madereva wenu wanawajueni zaidi kwakuwa muda mwingi mko nao" amesema Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango alipokuwa akizungumza jana na Wakuu wa Wilaya Jijini Dodoma katika Mkutano ulioandaliwa na Wizara ya TAMISEMI chini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Bi. Anjella Kairuki.

Chanzo Taarifa: Nipashe Radio One leo

Sasa na Wewe Mtani wangu Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mpango unataka Viongozi wasipige Story na Madereva wao je, Mimi GENTAMYCINE nitakuwa natoa wapi sasa Siri zao nyingi nyingi mpaka zile za Kiutendaji?

Hebu acha hizo bhana sawa? Tafadhalini Wakuu wa Wilaya na Viongozi Wengine hebu endeleeni kupiga 'Vistoristori' na Madereva wenu mkiwa ndani ya Magari yenu kwani mkinuniana Midomo yenu itanuka bure.

Imeisha hiyo!
 
Sahihi. Siri ni ya mtu mmoja. Yaan wewe mwenyewe. Usimwamini mtu mwingine zaidi yako
 
Mpango kama kiongozi alitakiwa ahamasishe maadili ya Utumishi wa Umma kudumishwa-Dereva nae ni mtumishi wa umma anapotoa siri za bosi wake hata za Ofisi anaweza kutoa pia.
 
Madereva wengi sana ni waongo na wambea hasa hawa wa viongozi nao wanajiona kama mabosi wao. Ukitaka kujua umbea wa madereva chunguza Tax Drivers na bodaboda.
 
Hawa viongozi wetu bure kabisa, kwa hivyo huyo Makamu wa Rais ameona hiyo ndio kero inayotusumbua sisi wananchi tusipate maendeleo?!.
Umeme kukatikaka kwake ni sawa maana line yake haina mgao wala kero ya maji!
Ajira watoto wake wana koneksheni!

Mungu tusaidie.
 
Miaka ya Mwalimu, madreva wengi wa makatibu wakuu, naibu katibu wakuu, makamishna, wakuu wa mashirika ya umma, mawaziri, naibu mawaziri walikua ni maafisa wa upelelezi waliopata mafunzo jeshini kabisa, lakini viongozi wengi walipewa madreva hao bila kuwafahamu, ikafikia hatua ya kuanzishwa leaders club, mwalimu akawa anashauri sana viongozi wawe wanaenda kunywa pale pako salama, wahudumu wakawekwa nyoka ukifanya vituko kesho yake mwalimu anakuhadithia vituko vyote ulivyofanya, basi sijajua kwa sasa mfumo ukoje wa hao madreva wa serikali za mitaa huko kama ni weledi au vipi,
 
Makamu wa rais anataka tusijue ubovu wa serikali wanayo iongoza? Tutajua tu, Tena tunajua mpaka nyumba ndogo za wakuu wa wilaya zilipo, michepuko ya mawaziri ni Nani etc.
Dereva Ni Kama mwanamke, atatunza Siri Sana Sana masaa 47.
 
Mabosi wenyewe wakitoka kwenye vikao wanaenda kulalamika kwa dereva. Utasikia "mimi mvumilivu sana, kuna pesa ilipigwa tukagawana sawa kwa sawa, kumbe mwenzetu alirudi kule akapiga nyingine kwamba sisi wote ndio tumemtuma. Sasa hivi mambo yameharibika tunatakiwa tulipe hela yote na aliyopiga yeye. Mimi silipi, kama bibi titi atanitumbua nitamwaga ugali."

"Yule mhindi mwoga sana. Yaani wenzangu wakitaka hela wanampigia tu simu kwamba tumetumwa kutoka juu utupatie milioni 20 uchangie mradi fulani. Na yule ni mwoga, anatoa tu ila analalamika kimyakimya maana hata kwenye event ya leo umemsikia maza mwenyewe katika shukrani zake hajamtaja yule mhindi kabisa, it means mchango wa mhindi jamaa zangu wamepiga" alisikika kiongozi mwandamizi akilalamika kwa dereva wake.
 
Watatuleteaje hapa kwenye jamiiforums bila kupiga nao story Wacha wajimalize wenyewe ...... "Yani unajua bwana Juma nchi hii bwanaaa ,,,,,,,,,,,,[emoji16][emoji28]"
 
Siri zao au hizo Stori zao ndio zinaendeleza au kudidimiza maendeleo ya hili taifa? Huyu mchumi kweli kawa mwanasiasa aliyeiva!
 
Back
Top Bottom