Dkt. Mpango: Wahubiri wa dini wanajilimbikizia mali

Dkt. Mpango: Wahubiri wa dini wanajilimbikizia mali

Uislam ulikwishalizungumza hili miaka mingi iliyopita!

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾

Enyi mlioamini! Hakika wengi katika Ahbaar (Mafuqahaa weledi wa Kiyahudi) na Ruhbaan (Monaki wa Kikristo) wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia Njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika Njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo.
-[Surat Tawba(9:34)]
Wewe nawe hizo ni hekaya za waarabu tu
 
Watakatifu Walimpiga Yesu hadi akatamka Mali zake zote alizojilimbikizia.. Yeye na Ukoo wake wote..

Pamoja na kutoa mbinu za kutokujilimbikizia MALI.. Bila shaka hao Watakatifu hawajamaliza kazi zaooo..

IJUMAA KUU10.jpg
 
Tena huyo huyo muha ndio asiongee kabisa bahili kama nini !! Sijaona kiongozi bahili kama huyo jamaa ! Mwisho asilete ujinga wa hekayq za makanisa apambane na ufisadi na wizi serikalini ,matririoni ya pesa wanakula wao na watoto ,wao Wana ukwasi wa kutisha !? Roho inamtoka kwa mia mbili mia mbili za mwamposa ,wakati nchi wanaitafuna na hajawahi kusema kitu? Hao maskini anaosema wanaibiwa amewahi kuwapa hata mia huyo bahili ! Anasema watu maskini kwani ninani kawafanya kuwa maskini
 
View attachment 3089684
Makamu wa Raisi Dkt. Philip Mipango

Makamu wa Raisi Dkt. Philip Mipango akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Kanisa la New Life Outreach iliyofanyika katika kanisa hilo Sakina mkoani Arusha amegusia suala la Wahubiri wa dini kujilimbikizia mali. Akieleza kuhusu jambo hilo Dkt. Mpango amesema:

“Hivi sasa yameibuka mafundisho ya viongozi wa dini yanayowaaminisha wafuasi wao kutegemea miujiza Zaidi ili kupata maendeleo badala ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Viongozi hao wanawaelekeza waamini wao kwenda kwenye nyumba zao za ibada ili wakaombewe wapate mali ikiwemo magari, nyumba, pesa wanazo zitamani, lakini pia wanaomba kutatuliwa shida zao tunashuhudia kuongezeka kwa wahubiri wanaojilimbikizia fedha na mali binafsi kutokana na sadaka na mauzo ya vitu mbalimbali vya hao watu wanyonge.
Wengi wa wahanga wa mahubiri ya aina hiyo ni wananchi wanyonge wanaokabiliwa na shida au matatizo mbalimbali ya maisha yakiwemo magonjwa, umasikini migogoro katika ndoa, ugumba kukosa ajira na kadhalika”
PIA SOMA
- Kwanini Serikali kupitia Wizara ya Nje, wasishirikiane na Wizara ya Nje ya Congo, kumkamata Tapeli alojiita Nabii kiboko ya wachawi?

- Nimeacha kutoa sadaka baada ya kusikia kauli hii ya mchungaji
Hawana kosa. Ujinga wa waumini ndio unaowarajirisha hao matapeli wa kiroho!
 
Uislam ulikwishalizungumza hili miaka mingi iliyopita!

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾

Enyi mlioamini! Hakika wengi katika Ahbaar (Mafuqahaa weledi wa Kiyahudi) na Ruhbaan (Monaki wa Kikristo) wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia Njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika Njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo.
-[Surat Tawba(9:34)]
Dini Zote Ni ujanja ujanja tuu
 
Back
Top Bottom