Dkt. Msonde anatumika katika kuwapiga "fix" walimu?

Dkt. Msonde anatumika katika kuwapiga "fix" walimu?

Mlalamikaji daily

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2014
Posts
744
Reaction score
1,621
Sijajua kwanini ,
Kwa manufaa ya nani!

Dk Msonde (naibu waziri upande wa elimu) anazunguuka nchi nzima kwa kile anachoita kuwasalimia walimu wenzake, lakini ndani yake kuna agenda ya kuwajaza matumaini HEWA walimu,

Na sana ni zile story za vifaranga vya kuku kunyonya kesho!
Iko hivi..

Baada ya serikali ya mwendazake kuwafanyia ukatili na dhuluma watumishi wa uma,

Dokta Msonde katika hizi ziara zake anawapiga fix walimu akisema yafuatayo

1. Serikali itafanya msawazo mwenyewe ameita hamornazition yaani kwamfano mtu aliajiriwa mwaka 2000
Kwasasa mwaka 2024 anatakiwa awe katika ngazi ipi ya mshahara?
Kwamba serikali itampa daraja hilo analostahili!

2. Kero za walimu zinatatuliwa kupitia mfumo wa TSCMIS..
Kwahiyo walimu wasiwe na wasiwasi,

HATA HIVYO Mpaka leo hii
Hakuna chochote kilichotokea bado watumishi wamedhulumiwa miaka 7 ,
Na anachosema msonde ni FIX

ANGALIENI HII VIDEO YA MSONDE MWAKA 2023

Huyo msonde katumwa na office kuu kuyafanya hayo coz wanajua walimu sisi ndio tutakaosimamia huo uchaguzi coz wakurugenzi washatemwa kisheria kusimami uchaguzi!!

Sasa mpango uliopo ni kuzirubuni minds za ndugu zangu matcha Ili wafanye favor Kwa ccm uchaguzi mkuu ujao!!

Namshukuru mungu Santa sijawahi kusimamia na sijawahi omba kusimamia huo ujinga uitwao uchaguzi uliplaniwa mshindi kabla ya kuhesabu kura!!!

Karma,Dola ,nature wakati ndio utawahukumu viongozi wadhalimu Kwa wananchi wao!!

Nina miliki KADI ya ccm lakini ukweli ni kwamba ujinga ndani ya chama umefika pomoni has ccm hii ya Sasa!
 
Umeandika Ukweli Mtupu, huyu MSONDE amewekwa kuwapooza Walimu baada ya Mh. Rais kushindwa kuahidi chochote kwa Waalimu siku ya Mei Mosi

Serikali imejaa Viongozi wasanii wanaowaona Waalimu Wajinga wajinga
 
Huu ndiyo ukweli halisi.

Taratibu ,sheria na kanuni hazifuatwi.
Watu wamebaki akili juujuu kusikiliza viongozi wameamka na kitu gani cha kuzungumza.

Ni bora mzazi ukamfundisha mwanao mfumo wa utumishi wa umma wa nchi hii mapema tangu akiwa mdogo kuliko ayakute haya maisha ya danadana katika utumishi wake.

Maisha ya utumishi wa umma hapo TANZANIA yametawaliwa na mihuri ya SIRI❌

Hakuna uwazi kabsaa na watumishi wanaishi kwa ndoto kama ombaomba.
Over...
 
Ndugu mwandishi hivi unajua utaratibu wa madaraja,daraja halipandishwi kwa walimu tu.msikilize vizur
 
Screenshot_20240525-203208.png
 
Na vishikwambi vyao fake havishiki netwok na vingi battery zimekufa haviwaki kabisa
Kwahiyo walimu mlitaka battery za vishikwambi zikifa serikali iwanunulie?

Kwa ujuha wa walimu, hizi fix zitawaingia tu.
 
Sijajua kwanini ,
Kwa manufaa ya nani!

Dk Msonde (naibu waziri upande wa elimu) anazunguuka nchi nzima kwa kile anachoita kuwasalimia walimu wenzake, lakini ndani yake kuna agenda ya kuwajaza matumaini HEWA walimu,

Na sana ni zile story za vifaranga vya kuku kunyonya kesho!
Iko hivi..

Baada ya serikali ya mwendazake kuwafanyia ukatili na dhuluma watumishi wa uma,

Dokta Msonde katika hizi ziara zake anawapiga fix walimu akisema yafuatayo

1. Serikali itafanya msawazo mwenyewe ameita hamornazition yaani kwamfano mtu aliajiriwa mwaka 2000
Kwasasa mwaka 2024 anatakiwa awe katika ngazi ipi ya mshahara?
Kwamba serikali itampa daraja hilo analostahili!

2. Kero za walimu zinatatuliwa kupitia mfumo wa TSCMIS..
Kwahiyo walimu wasiwe na wasiwasi,

HATA HIVYO Mpaka leo hii
Hakuna chochote kilichotokea bado watumishi wamedhulumiwa miaka 7 ,
Na anachosema msonde ni FIX

ANGALIENI HII VIDEO YA MSONDE MWAKA 2023

Walimu ujinga wanaulea wenyewe
 
Back
Top Bottom