Usipo sikiliza utajuaje kuwa ni takataka au siyo mkuu 'TUKANA'?
LOOoh!
Tena jamaa ni Doctor kabisa! Dr. Muchunguzi. Sijui ni Doctor katika vitu gani huyu, kuna anayejuwa atueleze?
Mazungumzo yote jamaa anajikanyagakanyaga tu, hakuna anachoeleza kikaeleweka!
Waalimu mtanisamehe, inawezekana huyu bwana alikuwa ni mwalimu. Wanafunzi wake walikuwa na shida kubwa sana.
Hapa inawezekana jamaa anapambania uteuzi!
Siwezi kuondoka kabla ya kumchambua kidogo huyu Daktari wetu jinsi nilivyo msoma:
1. Zungumza yake ya haraka haraka, unajuwa maana yake ni nini? Ni udhaifu, udanganyifu, kuvungavunga mambo; ili mradi aonekane anajuwa.
2. Lugha ya kimwili, aliyoiita mwenyewe 'body language'. Anaruka ruka sana anapozungumza. Mikono ipo kila sehemu. Macho na mdomo, vyote anavitumia kwa wakati mmoja. Hii ni kutaka kupoteza lengo. Kumfanya anayemsikiliza asiweke akili yake kwa yale anayoyazungumza, bali anavuta akili za msikilizaji kwa mambo yasiyo husika na kinachozungumziwa
3.' Incoherent'. Mtiririko wa anayozungumzia hayana mpangilio unaofuatana vizuri ili kujenga hoja inayoeleweka. Anashutumu, hapo hapo anaruka na kusema hamlaumu anayemshutumu. Huyu ndiye Daktari wetu.
4.Kujikomba/unafiki. hata haoni aibu
Wananchi wanao chagua wabunge wa namna hii, sijui wanavutiwa na kitu gani hasa!