Dkt. Muchunguzi: Kwenye maridhiano kama yetu, hatuhitaji upatanishi kutoka nje

Dkt. Muchunguzi: Kwenye maridhiano kama yetu, hatuhitaji upatanishi kutoka nje

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Maoni ya Dkt. Dennis Muchunguzi, Mkurugenzi Mkuu Taasisi za AFREDA na Rais wa Taasisi ya ACERICAANDO na Mtaalam wa maendeleo ya Kijamii na kiuchumi, mtaalam wa Lugha, maridhiano, upatanishi na ujenzi wa Amani



.Kwenye maridhiano kama ya kwetu haya, hatuhitaji upatanishi. Mara nyingi tumekuwa tukiita watu kutoka nje kuja kutupatanisha.

Mwaka 2007 pale Kenya, ulipoona Graça Machel, Kofi Annan, Mzee Mkapa, na baadaye alikwenda Jakaya Mrisho Kikwete, pale tulikuwa tunampatanisha Mheshimiwa Mwai Kibaki wa chama cha DP na Mheshimiwa Raila Amolo Odinga wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) ili waweze kukubaliana katika kuunda serikali. Ule ulikuwa ni upatanishi.

Zanzibar mwaka 2001, hivyohivyo, tulimleta mtu wa ngazi ya juu (alifeli). Unaona? Yule alifeli. Tunashukuru akina Mzee Mkapa na akina Kikwete walifanikiwa. Yule wa kwetu tuliyemleta mwaka 2001 Zanzibar alishindwa akaondoka. Ilichukua kumalizwa na ile kamati iliyokuwa imeundwa na Rais Mkapa ya akina Samia Suluhu Hassan, Ali Mohamed Shein, Brigedia Mwakanjuki na wengine.

Maridhiano ni upatanishi kama kuna watu wanaohitaji kupatanishwa. Maridhiano ya kwetu ni ya kitaifa, si ndiyo? Sasa unaposema namleta mpatanishi, najiuliza mpatanishi atakapokuja... kati ya waandishi wa habari wanaokwenda kuridhiana na Kanisa Katoliki, na machifu walioko Morogoro na Dodoma, mpatanishi anakuja kuwatanisha kitu gani? Wanafunzi wa vyuo vikuu na wachimbaji wadogo walioko Singida, anakuja kuwatanisha kitu gani? Najua unakolenga..."

Sasa kama kuna kitu kati yao na chama kilichoko madarakani, walipoketi mara ya kwanza Chadema na CCM, sikuona wamemleta mtu kutoka nje. Hawakumleta wakati ule Chadema ilipokaa na CCM. Lakini ACT-Wazalendo juzi imetia saini makaratasi na Chama cha Mapinduzi kule Zanzibar; sina uhakika kama wamemleta mtu kutoka nje. Sina uhakika.

Kwa hiyo, kama kuna imani hiyo, na kama kutakuwa na sababu kabisa za kuridhiana, si ndiyo? Kwamba ili mimi na wewe tuelewane, basi tumuite mpatanishi awepo kati yetu. Kama hautakuwa na hilo, mimi silipingi.
 
Kwenye ndoa, kosa dogo tunalimaliza wenyewe ila kosa kubwa tunalipeleka ukweni
 
Hili game wala haliitaji hasira wala kubishana....muda utaamua tu vizuri...kiburi cha watawala kitakomeshwa vema sana
 
Back
Top Bottom