mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dkt. Leonce Mujwahuzi amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuwa imara kutokana na kuwa na utaratibu mzuri wa kuchagua viongozi wake kwa utaratibu wa kuwabadilisha na kuchagua viongozi wapya kila baada ya muda fulani ambapo inapelekea viongozi hao kuja na maono mapya na ya tofauti katika kuongoza chama hicho.
Ameongeza kuwa, vyama vingine pamoja na taasisi vinapaswa kuiga mfano huo kwa kujenga utaratibu wa kubadili viongozi wao baada ya muda fulani ili kuendelea kuimarika na kuleta maono mapya katika uongozi wa vyama vyao.
Dkt. Mujwahuzi amesema hayo kupitia Kipindi cha Mizani cha TBC1 alipokua akichangia mada kuhusu tathmini ya Miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu kuanzishwa kwake pamoja na uelekeo wa chama hicho.