Nimeangalia kipindi cha Pambanua cha Channel Ten ambapo David Ramadhan alikiongoza akiwa amewakaribisha Dkt Sengodo Mvungi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Alex Mgongolwa wa Kituo cha Haki za Binadamu ambapo Dkt Sengodo Mvungi amedai kwamba mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ya kuanzisha "Nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" ni kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa sababu nchi ni Jamhuri ya Muungano na si vinginevyo. Kwa hiyo Jamhuri hiyo ilishavunjika tangu mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ambayo alidai kwamba "yalichomekewa!" Ni kwa sababu kulikuwa na swali kwenye kura za maoni: "Je, unataka mabadiliko ya Muundo wa Serikali baada ya uchaguzi wa Oktoba, 2010" ambalo alidai ni swali pana sana! Katika Orodha ya Mambo ya Muungano Dkt Mvungi alidai kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano nayo ni jambo la Muungano, kwa hiyo kuivunja Katiba hiyo ni kuvunja moja kati ya mambo ya Muungano. Pia amedai Wagombea wenza ni "batili" kwa sababu wanatoka "katika nchi nyingine!" Amedai kwamba saratani imeula Muungano wetu mpaka uko mahututi, tutafute suluhisho la kuachana na wazanzibari kwa amani tusije tukapigana. Tutapendana zaidi kuliko Wakenya na Waganda!
Kwa upande wa Alex Mgongolwa amedai kwamba tukae chini tutafute suluhisho kwa mazungumzo.
JK wetu ndio huyo hana habari kwamba hata urais wake wa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" haupo! Tujadili!
Mkuu
Buchanan, namkubali Prof. Mvingi kama msomi wa sheria aliyebobea kama ambavyo nitamkubali Prof. Mwakiembe, ila sizikubali comments zake kwenye baadhi ya issues kwa sababu yeye Mvungi, ameshajipambanua kushiriki siasa, na ndivyo ambavyo Prof. Mwakiembe atakavyo jipambanua kulinda mauza uza yote ya CCM.
Honest opinion kwenye hili, inatakiwa kutoka kwa wanasheria independent kama Prof. Shivji.
Kusu Zanzibar kuwa nchi ndani ya nchi, nilisema yafuatayo,
Zanzibar na Tanzania ni kama Baba na mwana. Wewe ndiye baba, unaitwa baba kwa sababu ndiye mkuu wa kaya, bread winner mwenye mamlaka yote.
Inapotokea mtoto wako umpendaye akaanza kulia kutwa kucha kwamba kwa nini ni wewe tuu unaitwa baba, na yeye anataka lazima aitwe baba, na kuendelea kulia kwa makelele mpaka unakosa amani, lakini wife alipomwambia 'nyamaza baba', ghafla alinyamaza na kuanza kufurahi sana, na yeye ameitwa Baba!, akamwambia mama na mimi ni baba. Jee wewe baba wa ukweli, utakasirika au kununa kuwa mwanao amechukua nafasi yako ya kuitwa baba, ama na yeye anataka kuitwa baba jina tuu lakini sio baba chochote, kwa vile powers za ubaba hana!.
Ndivyo ilivyo kwa JMT, Zanzibar kwanza walianza kwa kuomba bendera yao, wakapewa, kisha wakaomba wimbo wao wa taifa, wakapewa, kisha wale wagambo wao, (KMKM na JKU) kumpigia saluti rais wao, wakapewa, ndipo juzi wakajitwalia jina la 'nchi' na kuliingiza kwenye katiba ya Zanzibar ili hali kwenye katiba ya JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu tuu ya JMT. Jee JMT inasababu wa kuwakatalia kujiita majina yoyote inayoyataka hata wakiuita Falme za Zanzibar na kiongozi wao akawa Sultani Seif/Shein etc.
Zanzibar ni nchi kweli kama Zanzibar ndani ya Tanzania, kama mwanao atakavyoitwa baba ndani ya nyumba yenu, lakini nje ya nyumba, mwanao ni mtoto tuu, hana ubaba wowote mbele ya macho ya umma, ndivyo ilivyo nchi hii mpya ya Zanzibar, ni nchi jina tuu, haina uinchi yoyote mbele ya mataifa, ni nchi kwa maana ya eneo na jina tuu, isiyo na nguvu zozote za dola na za kinchi yaani sovereignty. Sasa unamashaka na jina tuu?.
Zanzibar nchi jina ndani ya muungano, sio nchi kimataifa na haina sovereignty!.
Pasco