nani kasema zanzibar si nchi? hebu tafuteni vizuri hizo kumbukumbu zenu ili mujue kuwa ni nchi au siyo. Hivi kama huyo Sengodo Mvungi anayewatia ujinga watanzania kwa kusema Zanzibar si nchi anajua vizuri Historia ya Zanzibar na Tanganyika na jinsi huo muungano ulivoanzishwa au anpiga kelele tu kwa vile kazizowea? Aliulizwa dola inatakiwa iwe na nini akasema mambo manne; 1:watu, 2:Uongozi wenye maamuzi, 3:Ardhi yenye mipaka, 4:kutambulika kimataifa. Swali linakuja hapa, je Zanzibar haina vitu vyote hivo? Kuna watu, viongozi, ardhi ambayo mipaka yake si ya kuwekwa na mtu(mzungu) bali ni mipaka iliyowekwa na mungu (bahari)na hilo la mwisho kama hajui historia ya zanzibar arudi asome tena, Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza kuwa na uwakilishi katika Umoja wa Mataifa, kabla hata ya Tanganyika kufikiria suala hilo. Sasa kama wanzanzibari wanadai nchi yao kisha wanaambiwa si nchi kwa misingi ambayo haipo kabisa, ni jambo la kushangaza sana. Sisemi kama muungano usiwepo, la ila wapeni wazanzibari kile wanachokidai bila kupiga makelele. Naamini watu wenye akili na wasomi kama hao kina Sengodo Mvungi wakikaa pamoja na kujadili na kukubaliana juu ya matakwa ya wazanzibari bac hayo ni mambo madogo na rahisi sana kutekelezeka, kama vile ilivokuwa rahic kwa baba yenu wa taifa kuunda muungano........!!!!