Hivyi ninyi mnamlalamikia nani?
hakuna kiongozi wa nchi hii ambaye anajali masuala ya muungano.
Dawa ni kwenda mahakamani kuishtaki jamhuri na serikali ya zanzibar kwa kutishia uhai wa UWEPO WA TANZANIA
Is that the way of dealing with the highest criminal act in the land (ie treason), by condoning it?
Wanaonyanyaswa ni Tanganyika ambao hawana serikali yao katika muungano. Na bado mambo yanageuzwa eti Zanzibar inanyanyaswa! Aidha serikali tatu au hakuna muungano. Ni hivyo tu.
mIMI KWA MAWAZO YANGU TURUDI KULE KULE KWA mWANZA SERIKALI TATU TANGANYIKA,ZANZIBAR NA MUUNGANO Sasa hapa ndo tujadili kwani Anayosema DK. Mvungi all is wright!! but Sisi ambao hatukusoma walalaloi tukipewa Khanga na T shirt basi CHochote anachotaka Mwenyekiti Ruksaa :mad2:
Znanzibar ni nchi mi nashangaa why hatuna Tanganyika yetu
Jumanne , 7 Septemba 2010 kuna mjadala iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee iliyotayarishwa Kituo cha sheria na haki za Binadamu kwa kushirikiana Kituo cha Huduma za Sheria cha Zanzibar.
Mada kuu:
* mapungufu yaliyoko katika katiba ya Jamhuri wa Muungano Tanzania ya Mwaka 1977
*Mabadiliko ya Kumi ya Katiba za Zanzibar.
Mjadala utaongozwa na mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuuu cha Dar Es Salaam na mada zitatolewa na mabingwa wa sheria na katiba.
SEE: Advert on Mwananchi, september 5, 2010, Page 5
nani kasema zanzibar si nchi? hebu tafuteni vizuri hizo kumbukumbu zenu ili mujue kuwa ni nchi au siyo. Hivi kama huyo Sengodo Mvungi anayewatia ujinga watanzania kwa kusema Zanzibar si nchi anajua vizuri Historia ya Zanzibar na Tanganyika na jinsi huo muungano ulivoanzishwa au anpiga kelele tu kwa vile kazizowea? Aliulizwa dola inatakiwa iwe na nini akasema mambo manne; 1:watu, 2:Uongozi wenye maamuzi, 3:Ardhi yenye mipaka, 4:kutambulika kimataifa. Swali linakuja hapa, je Zanzibar haina vitu vyote hivo? Kuna watu, viongozi, ardhi ambayo mipaka yake si ya kuwekwa na mtu(mzungu) bali ni mipaka iliyowekwa na mungu (bahari)na hilo la mwisho kama hajui historia ya zanzibar arudi asome tena, Zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza kuwa na uwakilishi katika Umoja wa Mataifa, kabla hata ya Tanganyika kufikiria suala hilo. Sasa kama wanzanzibari wanadai nchi yao kisha wanaambiwa si nchi kwa misingi ambayo haipo kabisa, ni jambo la kushangaza sana. Sisemi kama muungano usiwepo, la ila wapeni wazanzibari kile wanachokidai bila kupiga makelele. Naamini watu wenye akili na wasomi kama hao kina Sengodo Mvungi wakikaa pamoja na kujadili na kukubaliana juu ya matakwa ya wazanzibari bac hayo ni mambo madogo na rahisi sana kutekelezeka, kama vile ilivokuwa rahic kwa baba yenu wa taifa kuunda muungano........!!!!
Hakuna Effect yoyote ile ukitangaza Nchi moja iungane na Nchi nyingine ili mradi yawepo Makubaliano kati ya hizo nchi mbili zinazo ungana.Effect ya kutangaza nchi ndani ya nchi nyingine ni ipi?