Dkt. Mwakyembe aandika waraka wa siri!

Huu ni ****** na uzandiki mwingine wa mafisadi kupitia gazeti "lao" hili. Kama waraka huo umesambazwa kwa ndugu na jamaa na wananchi vipi uwe siri ya kutouanika na kutotaja undani wa waraka huo. Mwenyewe katoa tamko lake kwa maandishi moja kwa moja kwa vyombo vya habari vyote ili visimung'unye maneno au kupindisha - vipi leo chombo hiki kijifanye kinajua zaidi ya wanavyojua wengi - acheni kufanya biashara au kucheza siasa kwa mgongo wa afya za watu.
 
"Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa ndugu na marafiki wa karibu wa Dk. Mwakyembe vilisema kuwa, naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, amefikia hatua ya kuandika waraka huo kwa lengo la kutaka kuijulisha familia yake na taifa"

CDM=Tanzania Daima=Wazushi,waongo,Wanafiki
 

Waandishi wa Habari wa Tanzania na Wahariri wao ni wa kuwahurumia. Eti ni waraka wa siri; tena wanoa ndugu zake; tena gazeti linao; Sasa kuna siri tena hapo? Au ni majungu ya kuuzia magazeti?

Kwa suala la ajali ya Ihemi Iringa; Si kweli kwamba alipangiwa Lorry kwa sababu hizi hapa; Na kama uchunguzi wa Polisi kwamba ajali ile ni Uzembe wa Dereva, basi JF iandae wachunguzi binafsi wakafanye hata practice kuona kama kuna njama ilikuwepo.
1. Tanzania tunaendesha magari upande wa kushoto wa barabara (Left side of road driving);
2. magari yetu (na hata la Mwakyembe) ni Right hand driving (yaani Usukani upo Kulia mwa gari)
3. Ukitaka kulipita gari (kama siyo double ways kama barabara nyingi za Dar) lazima ulipite upande wake wa kushoto
Hivyo basi
1a. Kwa shimo aliloliingia dereva wa Mwakyembe pale Ihemi (kilomita 40 kutoka Iringa Mjini) lilikuwa upande wa kushoto (ukingoni) wa barabara (Ukitokea Mbeya) na kulia (ukingoni) wa barabara kama unatoka Iringa.
1b. Lile shimo lilikuwa pale kwa muda mrefu zaidi ya miezi minne (nililifahamu sababu nilikuwa na trip nyingi za maeneo ya Ifunda/Ihemi nikiendesha gari yangu
1c. Dereva wa Mwakyembe ni mzoefu na ile barabara kwa sababu amepita njia hiyo kwa muda mrefu hivyo alifahamu kama kabla ya kumaliza mteremko kuna shimo (tena kubwa kabisa siyo la kitoto)
1d. kama alitaka kulipita lorry kwa upande wa kushoto, huo ndo uzembe Klass 1.

2a. Mwakyembe alitoka Kyela jana yake jioni na kulala makambako kwa sababu walikuwa wamechelewa
2b. kwa kulala makambako walichoka na Hivyo mapema asubuhi walipoanza safari; mwakyembe alilala usingizi hadi wanapofika Ihemi (kilomita 120 kutoka Makambao)
2c. Dereva kwa uzembe naye alikuwa amelala (amesinzia) (hapa asitudanganye) kwa uchovu

3a. Ajali ingekuwa aligonga Lorry kwa nyuma ningekubali kwamba mwenye lorry alimtegeshe';
3b. Lorry kutosimama si hoja maana kuna ajali ngapi zinatokea na wengine wanaendelea na safari; watu wanaogopa kuuziwa kesi kama hii jamaa wa lorry angesimama basi angeuziwa kesi mbaya
3c. Askari waliomwokoa ndio waliotoa taarifa ya uchunguzi wa chanzo cha ajali kwa hiyo Mwakyembe hawezi kuwasifia kwa kumwokoa then akakataa taarifa ya uchunguzi wao wa ajali maana hawakuwa wanakwenda Njombe bali kwenye kituo chao cha kazi (barabarani) mara nyingi husimama Ifunda karibu na shule ya Sekondari.

Maswali ya kujiuliza
1. kama dereva alikuwa Oka na Mwakyembe mwenyewe; kwa nini hawakusoma namba ya usajili ya Lorry
2. Kwa nini basi hata wasikumbuke tu Lorry lilkuwa na rangi gani?
3. Kwa nini dereva wa Mwakyembe atake kulipita Lorry mteremkoni wakati sheria za usalama haziruhusu kupita gari katika mteremko mkali kama ule wa Ihemi?

Mhariri wa gazeti na waandishi wake wote hawana maana hata kidogo maana wameconcentrate kuleta historia ya ajali ya zamani badala ya kujuza walichodhani wangesema. huu ni Ujinga na umbumbumbu.

Kupewa sumu kwa Mwakyembe; Kwa vile anasema haikuwekwa kwenye chakula basi na kwa kuwa aliwekewa kwenye sabuni na kitambaa maalum cha kunawia kwenye chumba maalum ofisini kwake; Maana yake ni kuwa
1. Mhudumu wa ofisini kwake ndiye mhusika mkuu
2. Yule mtu wake aliyemwamini kuwa atamsaidia ofisini kwake (maana hana imani na wengine) ndiye aliyemwekea sumu
3. Kama hivyo vitu anatoka navyo nyumbani kwake maana ofisini kwake hawaamini; basi watu wa nyumbani kwake aliowaandikia huo wosia ndio waliomwekea sumu.

Pole Mwakyembe; lakini tunahitaji ukweli wa haya matukio kuliko kutumia matukio haya kujenga chuki. tunajua Mafia wapo lakini kwa nini iwe kwa kiasi cha chuki kujengwa hivi?
 

Hii report imekaa kama ile ya polisi waliyowahi kutoa.

Hapo kwenye BOLD inaelekea wewe ndiye Feleshi Mwenyewe yule DPP wetu, Karibu JF Afande!
 
3. Ukitaka kulipita gari (kama siyo double ways kama barabara nyingi za Dar) lazima ulipite upande wake wa kushoto
fafanua zaidi hapo..
 
Yani unataka ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe iwe hewani? Halafu ikishakuwa hewani wewe itakusaidia nini? Kikubwa unachotakiwa kujua ni kuwa AMEWEKEWA SUMU

Kama hataki ripoti ya ugonjwa wake ifahamike, basi akae kimya hakuna haja ya kupiga kelele kuwa amepewa sumu. Asubiri kifo tu kama wanavyokufa ndugu zetu wengine bila hata kufika India.
 
Every soul will taste death! (Quran 3:185)

Beware of those ho would do anaything to live forever.
 

Gazet la Uhuru je?
 



kama ni kujulisha Taifa mbona unawekwa kama siri wakati kasema ni kulijulisha Taifa? nadhani ni swala la kuwekwa hadharani kwani alishatoa ruksa kuwa lengo ni familia na taifa kupata habari

uongozi wa jf mpooooooooooooooooooooooooooooooozi
 
sijawahi kusikia moja kati ya dalili za ngoma ni ngozi kupukutika..get your facts right mkuu...basi hiyo ni aina mpya ya ukimwi

Ndugu yAngu wewe umekariri lazima ngwengwe ufe kwA madonda,au homa tuu.HatA MAfuaaaa yanakuapelekA kAmaa unayo,ni kwambA uakipAtA ugonjwA wowote na if hamnA defence mechAnism mwilini unakwendA nA maji.

Mimi nimekudokezA tuu,ilA kamA unAbishA AyA subiri.Time will tell mkuu
 
Tanzania Daima wanataka ukweli ufahamike. Ngoja tusubiri majibu ya Mwakyembe kama kweli kauandika waraka huo na yaliyomo. Tatizo haeleweki. Akinyamaza tunadhani karidhia? Kamjibu Manumba. Atasema angalau neno moja kuhusu waraka huu.
 

Endelea kumueliamisha NyAbhingi,maAnA ye kakAriri kuA ukimwi ampaakaA utoke mApele au kifuAa bAsi ndo unA ukimwi nA ndo itakAyokuonadoa..Hatabui kua ukimwi unakujA kwA dizaini nyingi,kama unao hata tumbo likikukamata unaondoka.Mi nimempA dokezo sasa kazi kwake kutAfiti
 
Wahindi wa Appollo hawajaligundua hili? Wanahangaikia nini sasa au ni biashara tu kwa kwenda mbele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…