Dkt. Mwakyembe: Kwa simba hii, sasa Tanzania tunaelekea kuwa kichwa cha muungwana, na si cha mwendawazimu

Dkt. Mwakyembe: Kwa simba hii, sasa Tanzania tunaelekea kuwa kichwa cha muungwana, na si cha mwendawazimu

Ngoja tusubir ya kina el masri, wyadad casablanca,... Ni swala la muda tu..... Tubakishe akiba ya maneno...
 
Waziri anafurahia simba kuwafunga wahabeshi hao wanywa kahawa?

Angetakiwa awe na kumbu kumbu kuwa kuna kipindi timu nzima ya wadjibout ilitoroka na haikurudi kwao hadi kocha.

Na afuatilia kuwa hawa waliopigwa nne wote wamepanda ndege kurudi kwao?

Kwenye suala la kuwapa wageni kipaumbele ni dhahiri kabisa huyu jamaa amezeeka na inabidi akapumzike.

Hivi anafahamu fitna za kwenye mpira?
Aende kwa waarabu aone kama atapewa hicho kipaumbele.( tusi la damange)

Na sijui magu anawatoa wapi watu kama hawa.
 
Djibouti kuna timu bana.

Tulipokuwa kwenye ubora wetu wa kikosi cha shilingi milion 200 tulikuwa tuliwapiga watu bao 8,6,5 kwenye preliminary round kama hii.

Hao wenye kikosi cha Bilion 1 na milioni 300 wameona wamefanya maajabu sana kushinda bao 4.


😀😀
 
Kiukweli Simba imecheza na ka timu kachovu sana! Ile timu hata ingecheza na Green Worriers ingechezea nyingi tu! Simba inapaswa ijipange haswa isibweteke na sifa za kipuuzi!


Najua hatua ya pili watakutana na AL MASRY SC ya Umisri, hapo ndio utakuwa mwisho wao kwenye ngazi hii ya soka.

Aristide BANCE

Islam SALAH

hawatowaacha Bilioni 1.3 salama.
 
Ngoja tusubir ya kina el masri, wyadad casablanca,... Ni swala la muda tu..... Tubakishe akiba ya maneno...


Ndio maana nikasema simba akimalizana na wakulima wa kahawa anakutana na Mwanaume wa Kimisri AL MASRY SC.

Na ukuta ule wa simba naona jamaa wakila tende gizani. 😀😀😀
 
Waziri Wa michezo anaonesha mahaba kwa timu moja huku nyingine anaibagua.

......huyu Mzee muda Wa kupumzika umefika anakoenda anazidi kujishushia heshima.
Anaonesha kiwango chake cha kutofahamu kandanda. Simba imecheza na Mafundi Gereji wa Djibout, tayari waziri anamwagika maneno mfululizo...wakati Simba inadundwa na Green Warriors waziri alikuwa nani?
 
Back
Top Bottom