Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga amezungumzia kuhusu matumizi ya Artificial Intelligence (Akili Unde), msikilize akifafanua jinsi gani suala hilo linavyoweza kuwa hatari kwa Jamii...
Korea ya kusini kupitia taasisi ya usalama mtandani ya korea- KISA,inatarajiwa kuendesha mafunzo ya siku tano kwa watalaamu wa masuala ya uhalifu mtandanoni wa Tanzania, ikiwa ni katika kupunguza changamoto ya uhalifu mtandaoni kupitia akili unde ambao unatajwa kukua kwa asilimia 30 kila mwaka .
Mafunzo hayo ambayo yanafanyika jijini Dar es salaam yakihusisha watalaamu 33 kutoka sekta binafsi na za umma kupitia tume ya Tehama nchini ICT yanatajwa kama sehemu ya kimkakati ya kuongeza watalaamu wa kukabiliana na uhalifu mitandaoni ambapo kwa mujibu wa mkurugenzi wa Tume hiyo, Dokta Nkundwe Moses Masaga bado wanahitajika kwa wingi kulingana na kasi ya ukuaji wa matumizi mtandaoni .
Kwa upande wake mtafiti kutoka taasisi ya usalama wa mtandao nchini Korea –KISA, Kim Minyoung amesema kwa sasa dunia inakabiliwa na changamoto ya uvamizi wa mitandao, kupitia teknolojia ya akili unde hivyo kuna haja ya kuwa na kundi la watalaamu wa uhalifu mtandaoni hivyo wameamua kuwezesha mafunzo hayo ambayo yatafanyika zaidi ya mataifa 70 duniani huku kati ya hayo mataifa 50 ni Afrika .
Pamoja na masuala ya uhalifu mtandaoni pia mafunzo hayo yanatarajiwa kuangazia namna ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na ujio wa akili unde hususani eneo la utoaji taarifa potofu jambo ambalo linasumbua mataifa mengi.