Dkt. Mwigulu ameanza kujipigia debe kwa kasi tena

Dkt. Mwigulu ameanza kujipigia debe kwa kasi tena

Mnambua

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2020
Posts
246
Reaction score
233
Jumamosi iliyopita kulikuwa na msiba kwenye makao makuu ya kata anayotoka Dkt. Mwigulu kule Kyengege - Iramba. Basi Dkt. Mwigulu bila kutoa taarifa yeyote au kuomba ruhusa ya kutoka nje ya Dodoma akakimbilia msibani kwa gari la Ofisi - Msibani gari lake limeandikwa W- KS utafikiri aliyefariki alikuwa ni mfanyakzi wa ofisini kwake. Akiwa msibani akateta na baadhi ya watu akiwepo Msaidizi wa Askofu wa KKKT ambaye alimpigia debe kiaina. Uzuri kila afanyalo tunalirekodi na kuwasilisha chamani. Na asipozidisha umakini ajue anajiponza.

Basi baada ya kuteta naye huyo Bwana Msaidizi wa Askofu Dkt Mwigulu akaulizwa kama atakuwa na la kuongea, akasema hana isipokuwa atasalimia tu ili asionekane kama kaanza Kampeni. Yule Bw. Msaidizi wa Askofu akamwambia Dkt. Mwigulu kazi ya kupiga debe hapo ataifanya yeye. Na kweli baada ya Dkt. Mwigulu kusalimia kwa muda wa takribani dakika mbili hivi - yule Bwana Msaidizi wa Askofu akaanza kumnadi Dkt Mwigulu "Mheshimiwa wewe unaogopa kusema ila mimi nakuhakikishia kuwa huna haja hata ya kupiga kampeni tena kwa sababu Mwaka huu Tayari Mwenyezi Mungu ameshakuchagua. Utaendelea kuwa Mbunge na wote hapa tunakuhakikishia hilo"

Wengine tukabaki midomo wazi!

JF mtaona huu ni umbeya lkn ni umbeya wenye maana!
 
Tushazoea majungu yenu, mnaishi kwa kuwindana tu.
Aombe ruhusa ya kutoka Dodoma au asiombe inatuhusu nini? Mangapi yanayofanyika yanaonyesha matumizi mabaya ya Ofisi au vifaa vya Ofisi?
Hilo jimbo mpk mtatoana roho!

Sent using kidole gumba
 
Niliongea na watu wanaonikusanyia mazao kuanzia makunda, tumuri, kyengege, kizaga, misigiri, tyandu kiukweli walinieleza mwigulu hana mpinzani huko atashinda na wanampenda hivo naona huko wengine mnapoteza tu muda wenu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Niliongea na watu wanaonikusanyia mazao kuanzia makunda, tumuri, kyengege, kizaga, misigiri, tyandu kiukweli walinieleza mwigulu hana mpinzani huko atashinda na wanampenda hivo naona huko wengine mnapoteza tu muda wenu


Sent from my iPhone using JamiiForums
Unasema kweli lkn sasa ukipendwa sana usianza kukufuru. Kuna wengine tu hawajajitokeza wakijitokeza wanaweza kubadili upepo ghafla. Asijiamini!
 
Iramba mna nyumba nyingi sn za tembe, hivyo lazima atapita maana watu siku hiyo watakula wali na nyama + pombe
Kweli ni nyingi na zimesababishwa na Dkt. Mwigulu!
 
Haāhaa Yaani wana CCM mnafikiri kweli Mwigulu hata akicheza rafu za aina gani kwenye chama mnaweza kumtema eti asipate ubunge kama jiwe ameshamkubali? Mnafikiri kuna kuchukuliwa hatu8ia kwa confidant wa Magufuli kweli? Magufuli huyu huyu aliyewatangazia CCM Kongwa kuwa yoyote atakayempinga Ndugai kwenye kura za maoni za Ubunge mwaka 2020 kuwa asahau kuteuliwa? yaani kwa kifupi ni kuwa, wale watu wa karibu na Rais hawa wanatakiwa washinde ubunge kwa njia yoyote, iwe kuvuynja kanuni ama la
 
CCM hoyeee.. Mwigulu safiii na lazima apite mheshimiwa Mwigulu tunamuunga mkono maana Ni mteule wa Raisi nyie wengine mtavuna mabua na kupika majungu mpaka akili ziwakae sawa.. "Mwimbo Ni mmoja tu, Mwimbo wa sifa"
 
Tushazoea majungu yenu, mnaishi kwa kuwindana tu.
Aombe ruhusa ya kutoka Dodoma au asiombe inatuhusu nini? Mangapi yanayofanyika yanaonyesha matumizi mabaya ya Ofisi au vifaa vya Ofisi?
Hilo jimbo mpk mtatoana roho!

Sent using kidole gumba
Kweli hata wa kumuomba hayupo yupo kwake hukooo mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piga ua ni Professor Kitila Mkumbo alie safi na hajawahi iba jina asome sekondari.
 
Back
Top Bottom