Dkt. Mwigulu ameanza kujipigia debe kwa kasi tena

Nimesoma maelezo yako na kuconvert kuwa video, kwa mujibu wa sheria za ugambani na tamaduni, hiyo siyo offside kabisa bali ni majungu tu ya ninyiem. Pyeeep mpira uwekwe ulipoishia ili mparuane.
 
Jumamosi iliyopita kulikuwa na msiba kwenye makao makuu ya kata anayotoka Dkt. Mwigulu kule Kyengege - Iramba. Basi Dkt. Mwigulu bila kutoa taarifa yeyote au kuomba ruhusa ya kutoka nje ya Dodoma akakimbilia msibani kwa gari la Ofisi - Msibani gari lake limeandikwa W- KS utafikiri aliyefariki alikuwa ni mfanyakzi wa ofisini kwake. Akiwa msibani akateta na baadhi ya watu akiwepo Msaidizi wa Askofu wa KKKT ambaye alimpigia debe kiaina. Uzuri kila afanyalo tunalirekodi na kuwasilisha chamani. Na asipozidisha umakini ajue anajiponza.

Basi baada ya kuteta naye huyo Bwana Msaidizi wa Askofu Dkt Mwigulu akaulizwa kama atakuwa na la kuongea, akasema hana isipokuwa atasalimia tu ili asionekane kama kaanza Kampeni. Yule Bw. Msaidizi wa Askofu akamwambia Dkt. Mwigulu kazi ya kupiga debe hapo ataifanya yeye. Na kweli baada ya Dkt. Mwigulu kusalimia kwa muda wa takribani dakika mbili hivi - yule Bwana Msaidizi wa Askofu akaanza kumnadi Dkt Mwigulu "Mheshimiwa wewe unaogopa kusema ila mimi nakuhakikishia kuwa huna haja hata ya kupiga kampeni tena kwa sababu Mwaka huu Tayari Mwenyezi Mungu ameshakuchagua. Utaendelea kuwa Mbunge na wote hapa tunakuhakikishia hilo"

Wengine tukabaki midomo wazi!

JF mtaona huu ni umbeya lkn ni umbeya wenye maana!
Kitila is watching.
 
Nilifikiri ameshaanza kupaka rangi kwenye mawe..Raisi mtarajiwa wa kwenye mawe...😀

Everyday is Saturday.......................😎
 
Piga ua ni Professor Kitila Mkumbo alie safi na hajawahi iba jina asome sekondari.
Mwambieni Prof apige kazi apunguze siasa. Kwa nafasi yake yeye kama mtendaji mkuu wizarani, hapaswi kushinda JF kujipigia promo. Asubiri Kuna Wabunge kumi wa kuteuliwa na Rais, tutampa nafasi moja.
 
Jumamosi iliyopita kulikuwa na msiba kwenye makao makuu ya kata anayotoka Dkt. Mwigulu kule Kyengege - Iramba. Basi Dkt. Mwigulu bila kutoa taarifa yeyote au kuomba ruhusa ya kutoka nje ya Dodoma akakimbilia msibani kwa gari la Ofisi - Msibani gari lake limeandikwa W- KS utafikiri aliyefariki alikuwa ni mfanyakzi wa ofisini kwake. Akiwa msibani akateta na baadhi ya watu akiwepo Msaidizi wa Askofu wa KKKT ambaye alimpigia debe kiaina. Uzuri kila afanyalo tunalirekodi na kuwasilisha chamani. Na asipozidisha umakini ajue anajiponza.

Basi baada ya kuteta naye huyo Bwana Msaidizi wa Askofu Dkt Mwigulu akaulizwa kama atakuwa na la kuongea, akasema hana isipokuwa atasalimia tu ili asionekane kama kaanza Kampeni. Yule Bw. Msaidizi wa Askofu akamwambia Dkt. Mwigulu kazi ya kupiga debe hapo ataifanya yeye. Na kweli baada ya Dkt. Mwigulu kusalimia kwa muda wa takribani dakika mbili hivi - yule Bwana Msaidizi wa Askofu akaanza kumnadi Dkt Mwigulu "Mheshimiwa wewe unaogopa kusema ila mimi nakuhakikishia kuwa huna haja hata ya kupiga kampeni tena kwa sababu Mwaka huu Tayari Mwenyezi Mungu ameshakuchagua. Utaendelea kuwa Mbunge na wote hapa tunakuhakikishia hilo"

Wengine tukabaki midomo wazi!

JF mtaona huu ni umbeya lkn ni umbeya wenye maana!
Hongera sana Mh waziri wa KS na mpe pole sana Bwana KM.
 
Back
Top Bottom