Dkt Mwigulu Nchemba akishinda itakuwa ni kwa sababu wa wapiga kura wale wasiobadilika na hasa wale maskini ambao wanaishi nyumba za tembe na anaowanunulia pombe. Bei ya pipa la pombe Iramba ni shilingi laki moja na nusu- Ina maana Dkt Mwigulu akinunua mapipa mawili ya pombe kwa kila kijiji tayari ana wapiga kura wengi. Kwa hakika kwa jimbo la Iramba analotoka Dkt. Mwigulu hamna watu makini na waliosoma wanaomkubali. Napafahamu Iramba nilipoanzia kazi na bahati nzuri nimeoa huko Dkt. Mwigulu kwa sasa hana jipya wa Wanyiramba anawatumia kama ngazi tu ili kutimiza azma yake, ubunge kwake sio kitu tena!