Dkt. Mwigulu: Idadi ya Benki imepungua nchini, zimebaki 45

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi Desemba 2022 kulikuwa na benki 45 ikilinganishwa na benki 46 katika kipindi kama hicho mwaka 2021.

Amesema Kupungua kwa idadi ya benki kulitokana na Exim Bank Limited kuinunua benki ya First National Bank Tanzania.

Hata hivyo, amesema matawi ya benki yaliongezeka hadi 998 mwaka 2022 ikilinganishwa na matawi 990 mwaka 2021.

“Hadi Desemba 2022, amana za wateja zilifikia Sh32.5 trilioni kutoka Sh28.5 trilioni katika kipindi kama hicho mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 14.1,”amesema.

Hayo ameyasema leo Alhamisi Juni 15, 2023 akisoma Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2022 iliyowasilishwa Bungeni jijini Dodoma.

BUNGENI
 
Hilo nalo lina umuhimu gani? Au basi nendeni mkalitizame
 
Kuna Benki moja tu ya Maana ambayo imefungwa Speed Governor hence kufanya maisha kuwa magumu....

Miamala ya Kwenye Pesa (kwa kuweka Tozo zisizo na Busara wala akili ambazo wala hatuoni faida ya value for money)

And that is on him na genge lake...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…