Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kwamba kuanzia July 01, 2023, iwe ni marufuku kwa Taasisi yoyote ya Serikali kufunga biashara, ofisi ama maeneo yoyote ya uzalishaji kwa kigezo cha kukiuka taratibu mbalimbali.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kumekuwepo na vyanzo vikubwa vya adhabu ambavyo hutumika kama vyanzo vya mapato na kuwepo kwa kaguzi nyingi zisizokuwa na tija hivyo kuongeza usumbufu katika kufanya biashara hali hii inasababisha serikali kupokea malalamiko kutoka kwa wawekezaji na Wafanyabbiashara kuhusu kuongezeka kwa gharama za uzalishaji na uwekezaji na ufanyaji wa biashara.
Utafiti unaonesha kuwa kaguzi nyingi zinafanyika kutafuta makosa badala ya kuongeza tija, kaguzi hizi zinafanywa na Taasisi mbalimbali kila moja kwa wakati wake hivyo Wafanyabiashara kutumia muda mwingi kupokea wageni badala ya kujihusisha na shughuli za uzalishaji na utoaji huduma.
Adhabu kubwa zinasababisha Biashara kufanyika kwa hasara, ukubwa wa adhabu unaotoa fursa za majadiliano na hivyo kuipotezea serikali mapato. Adhabu zinatumika kama chanzo mapato kwa taasisi za udhibiti na kutokuwepo kwa mfumo jumuishi wa kuzilipa.
Katika kutatua kero hizo napendekeza kuanza kwa mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa ada (Single Window Payment system na taasisi za udhibiti kuweka utaratibu ambao hautasababisha usumbufu kwa Wafanyabiashara bila kuathiri majukumu ya msingi ya Taasisi hizo napendekeza hatua hizo zianze mara moja mwaka wa fedha 2023/24.
UFUNGAJI WA BIASHARA
Ufungaji wa biashara kwa sababu zozote zile una atharii kubwa kwa ustawi wa uchumi wetu na unaathiri ajira za Wananchi, Ustawi wa biashara, kampuni pamoja na mapato ya serikali. Aidha, utaratibu huu unakwenda kinyume na jitihada anazozifanya Rais Samia za kuboresha mazingira ya biashara hapa nchini.
Ili kuondokana na athari hizi, napendekeza kuanzia tarehe 1/07/ 2023 iwe ni marufuku kwa taasisi yoyote ya Serikali kufunga biashara, ofisi au maeneo yoyote ya uzalishaji kwa kigezo cha kukiuka taratibu. Aidha napendekeza sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zirekebishwe ili kumchukulia hatua mwenye biashara kwa makosa ya biashara na siyo kuifunga biashara yenyewe, hatua hii inalenga kulinda ajira za watanzania, mapato ya biashara, kukuza uchumi na kuongeza mapato ya Serikali.
Kufunga biashara badala ya kumchukulia hatua anayefanya biashara ni hatua ya kikatili dhidi ya biashara na shughuli za uzalishaji. Hatua hii inalenga kulinda biashara za Watanzania, mapato ya biashara, ukuza uchumi na kuongeza mapato ya serikali.