Dkt. Mwigulu L.N, (Phd) Pitia haya utapata jambo fulani muhimu

Umeelezea vizuri sana.

Hili baadhi ya wakaguzi wameshaliona, ni vile baadhi ya mapendekezo huwa hayafanyiwi kazi na serikali.

Unakuta gharama za ufuatiliaji wa mradi wa m15 ni M 30. Inauma sana.
 
Ila chukua muda kidogo umuelewe Mwigulu ni mtu wa aina gani itakusaidia
 
Umeandika mengi lakini ulimuandikia ndiyo jangili no 1, nenda Wizara ya fedha uone watu wanavyojilipa Honorarium za kufuru mpka milioni 14 kwa mwezi kwa Afisa wa kawaida sn
Hawa hawarambi tena asali hawa wanakunywa madumu ya Asali
 
Kiongozi, umeongea ukweli mchungu, watumishi wa Umma wanakandamizana wenyewe kwa wenyewe!

Fikiria kama ulivyosema, waalimu walihusika kusimamia miaradi ile, na bado hawakupata posho, unakuta jamaa katoka huko mkoani au wizarana, anakuwa mkali, baada ya hapo anaenda kusaini posho, mwalimu anabaki na maumivu ya matusi na umaskini
 
Ila chukua muda kidogo umuelewe Mwigulu ni mtu wa aina gani itakusaidia
Tunaandika haya, kwa Mwigulu, ingawa bado taasis nyeti inawezayachukua na kufanyia kazi ikiona yanafaa.

Hivyo hata asiposoms yeye, bado vyombo vyenye mamlaka fulan vinaweza kuyachukua na kufanyia kazi.
 
Pesa ni zinapigwa wazi wazi...
Kinachouma ni kuwa, tunatumia njia/ mifumo ya kizamani, hatutaki kubadilika kuendana na uhalisia wa nchi yetu!

Kwanini Kenya wakiamuaga yao wanafanya, kwanini sisi Tanzania ??

Pesa inayopotea kwenye mikono ya watu ni nyingi sana,
 
Ukiingia kwenye system na uone pesa zinavyopigwa bila uoga utaingiwa na hasira...

Wewe unakamuliwa kodi, wengine wanaenda kuchungulia zimeingia ngapi wanachukua kama zao...
 
Kaka yangu Mwigulu L Nchemba (Phd).
Naona hujui.

Unapoweka jina la mhusika likitanguliwa na Dr.; huweki tena Ph.D. baada ya jina lake.

Hapa mtambulishe kama Dr Mwigulu tu basi; au Mwandike kama, Mwigulu Nchemba, PH.D.

Na sijui kama Mwigulu ndilo jina lake la ubini, au Nchemba? Kama ni Nchemba, basi atafahamika kama Dr Nchemba, au Mwigulu Nchemba, PH.D.
 
Asante kwa kunisahihisha! ingawa dhumuni la mada linaeleweka...
 
Kinachouma ni kuwa, tunatumia njia/ mifumo ya kizamani, hatutaki kubadilika kuendana na uhalisia wa nchi yetu!

Kwanini Kenya wakiamuaga yao wanafanya, kwanini sisi Tanzania ??

Pesa inayopotea kwenye mikono ya watu ni nyingi sana,
EeeenHeeee,

Usilojua bhwanah, unawasifu Kenya?
 
Asante kwa kunisahihisha! ingawa dhumuni la mada linaeleweka...
Sijakusoma huko ndani ulichoandika mkuu Lubengera. Mimi niliishia huo mstari tu wa kwanza. Huwa ni mvivu kusoma maandiko marefu hapa JF, labda iwe ni jambo linalonivutia kuchukua muda kufanya hivyo.
 
Sijakusoma huko ndani ulichoandika mkuu Lubengera. Mimi niliishia huo mstari tu wa kwanza. Huwa ni mvivu kusoma maandiko marefu hapa JF, labda iwe ni jambo linalonivutia kuchukua muda kufanya hivyo.
Ok,
 
Yes, nawasifu kwakuwa wanafanya vizuri! mfano mzuri ni aina yao ya elimu wanayotoa sasa ivi!
Aaah, sikujua kuwa huko ndani ya mada yako kuna maswala hayo ya elimu, ambayo kiuhakika nami nitaungana nawe katika hili.

Nilihusisha kuwasifu kwako na mambo ya fedha, ufisadi. Ninaelewa kiasi kuhusu udhaifu wao katika eneo hili.
 
Tumekuwa wagumu sana wa kufanya mabadiliko anuai yanayoendana na wakati, mazingira na hali tuliyonayo kama Watanzania.

Moja ya sehemu inayopoteza fedha nyingi za Serikali ni pamoja na eneo la ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi.
 
Ngoja niungane nawe katika kuwasifu wakenya katika eneo jingine walilofanikiwa zaidi hivi karibuni, wakati sisi tukididimia zaidi upande huo.

Pamoja na kusemekana kuwepo na mkataba mbaya, uliolazimisha kuweka rehani bandari yao ya Mombasa, lakini jinsi ilivyojengwa kwa uharaka na kuanza kufanya kazi bila kupoteza muda ni jambo zuri sana.
Sasa linganisha hali hiyo na huku kwetu; kipande tu cha kutoka Dar hadi Morogoro, hata haifahamiki kitakuwa tayari lini. Na hakuna anayesema kwa uwazi tatizo ni nini hasa!

Mchina huyo huyo, kajenga hii barabara iliyofunguliwa juzi ya Nairobi Express itokayo JKIA hadi mjini katikati. Imejengwa na kukamilishwa katika nusu ya muda uliopangwa! Mimi sijui kama kuna mradi wowote hapa nchini kwetu uliofanyika na kukamilishwa bila mizengwe.

Matokeo yake ni kwamba miradi hii inapokamilika haraka, hata uchangiaji wake katika pato la nchi unaonekana bayana, na ndiyo maana miradi mingi iliyofanyika hivi karibuni Kenya imechangia sana katika kukuza pato lao la nchi, tofauti kabisa na sisi.
 
Una maana mleta mada naye anatafuta asali?

Imenilazimu kusoma andiko lake baada ya kujibishana naye; lakini nilishindwa kulisoma lote baada ya kuona mwelekeo wake ulivyo. Sijui kama kuna mapendekezo yenye tija. Ningedhani ingekuwa bora kwake kuhimiza watendaji wafuate taratibu zilizopo katika utendaji kazi wao.
 
Asante mkuu Kalamu, nadhani bado Kwetu tuna tatizo sehemu! linapokuja suala la maamuzi huwa ni tatizo sana.
Naona gape la pato la taifa kati yetu na kenya linazidi kuwa kubwa, wapi tunashindwa hasa sisi??

Kenya wanafanya vizuri sana maeneo mengi, hata upande wa uhuru wa mahakama, Biashara, na technolojia.

Nilikuwa naangalia hata uwekezaji bado wanatupiga gape kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…