Dkt. Mwigulu L.N, (Phd) Pitia haya utapata jambo fulani muhimu

Dkt. Mwigulu L.N, (Phd) Pitia haya utapata jambo fulani muhimu

Una maana mleta mada naye anatafuta asali?

Imenilazimu kusoma andiko lake baada ya kujibishana naye; lakini nilishindwa kulisoma lote baada ya kuona mwelekeo wake ulivyo. Sijui kama kuna mapendekezo yenye tija. Ningedhani ingekuwa bora kwake kuhimiza watendaji wafuate taratibu zilizopo katika utendaji kazi wao.
Taratibu zilizopo ni za hovyo, ndio mana nimeegemea kwenye upotevu wa fedha katika ufuatiliaji.

Nimetoa mfano flan wa mradi wa 45 M.

unavyosema hizi taratibu, basi ni haki kwa watendaji kufanye yale yaliyoko kwenye taratibu, ikiwemo kulipana posho hata kwenye kazi ambazo hazifai kulipwa posho.
 
Kaka yangu Mwigulu L Nchemba (Phd).

Hoja hizi hapa chini, ni baada ya kuongea na wewe (siku x) baada ya kusoma bajeti.

Hongera sana kwa kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Ukweli umejitahidi sana kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na ninaona lengo lako ni viewable kabisa. Hongera kwa Mama (Hon S.S.H).

Mawazo yangu, yatajikita hasa kwenye eneo la ufuatiliaji wa fedha za serikali, nitajitahidi kuwasilisha kwa kurejea mifano ya kawaida isiyokuwa na rejea maalumu ya nyaraka, video au ushahidi wowote kutoka serikalini, hii ni kufanya mada yangu kuwa huru katika uchangiaji bila ya kuathiri upande wowote au mtu yoyote aliyeko kwenye mamlaka au kumdhania mwandishi husika, (Mawazo nitayawekakatika hali ya ukawaida sana)

1. Nianze na Aina ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ukaguzi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa (PCCB).

Dr, M.L N, ukaguzi wetu umekuwa wa kuvizia watumishi, na hii imepelekea kutokuwa na tija ya ukaguzi hasa kwa dunia ya sasa ivi, Kuna haja ya kubadilisha aina ya ukaguzi tulio nao, ninafaham kuna standard za kimataifa, lakini kwa uzoefu wangu katika ukaguzi, modality ya ukaguzi haiathiri uwasilishwaji wa taarifa ya ukaguzi kama ilivyo katika hadidu za ukaguzi na standard za kimataifa.

Fedha nyingi sana zimekuwa zikitumika katika kufuatilia fedha kidogo ziizoko kweye miradi,badala ya fedha kidogo kufuatilia fedha nyingi zilizoko katika miradi, hali hii husababisha fedha za miradi kuwa kidogo(mfano niliwai kutembelea mradi mmoja wilaya flani. Mradi ule ulikuwa wa Tsh 45m, lakini taarifa nilizozikuta pale ni za ajabu kweli kweli (Eti Wizara Ilikuwa inaufuatilia, RAS alikuwa anaufuatilia, PCCB, PPRA na CAG)na mwisho wake mradi ule kwa taarifa ya CAG ni kwamba haukidhi viwango vilivyohitajika na hivyo kupendekeza watumishi husika kuchukuliwa hatua za kinidhamu, Tujiulize kwapamoja, zile timu zote zilizokuwa zinatembelea pale hazikuona mapungufu hayo, je kama CAG angeshiriki mapema hali ya uduni huo ungejitokeza?? Mh Waziri vyombo nilivyovitaja ni muhimu sana katika usimamizi wa fedha za umma, ila nashauri nao kushiriki direct na kutoa ushauri kadri mradi unavyotekelezwa. Gharama za kusuburi mradi kuisha kwa kiwango duni husababisa gharama maradufu ya mradi huo kama kusimamisha watumishi, gharama za ufuatiliaji, eg Posho, mafuta etc

Ukaguzi una amini kuwa mwanadamu huwa ana utimamu wa akili kwa 100% kwa kipindi cha mwaka mzima, na hivyo maamuzi yoyote yafanywayo Ofisini iwe kwa bahati mbaya au kwasababu ya msongo wa mawazo , mkaguzi huamini jambo hilo lilifanyka kwa makusudi.

Tatizo la afya ya akili kwa sasa limekuwa kubwa sana na ndio mana nchi zilizo endelea tayari wameanzisha mitaala juu ya elimu ya afya ya akili (Marekani ni mfano wake) hii ni baada ya kuona kuwa watu wamekuwa wakifanya mambo yasio sahihi na kuhukumiwa pasipo kupimwa afya ya akili.

Nini Kifanyike.

a. Vyombo vya Usimamizi katika maeneo yao ya kazi, wawe jicho la pili la kila kinachoendelea katika ofisi za Umma na kutoa ushauri stahiki kwa wakati kuliko kusubiri mwisho wa mwaka, ambao wakaguzi hugeuka kuwa Miungu watu na kuogopwa hata kwa mambo yaliyofanyika kwa gharama za afya ya akili, mazingira duni ya kazi, msongo wa mawazo sababu ya maisha duni ya watumishi, kutokukubali utetezi wa muhusika aliyeababisha hoja.

b. Sio kosa kuanzisha aina ya ukaguzi ambao utaendana na wakati huu ambapo dunia imekuwa katika mabadiliko ya Sayansi na Elimu, mfano mzuri ni jirani zetu wa Kenya, baada ya kufanya mabadiliko ya Elimu yao ambayo imekuwa CBC kwa sasa(competency based curriculum), sasa Benki ya Dunia imeitambua Kenya Kuwa na elimu bora katika Bara la Afrika.

c. Katika hali ya kawaida, mwanadamu hawezi kukaa mwaka mzima bila kufanya kosa, hivyo taasis mbali mbali zimekuwa zikitulaumu baadhi ya wakaguzi kutokutenda haki, ili kuepuka hili, naishauri serikali kuanzisha mfumo wa wakaguzi utakaokuwa una monitor mamuzi ya watumishi hasa wa fani za Uhasibu na Manunuzi kuepuka ubadhirifu.

d. Fani ya ukaguzi kuwa na wataalamu wengi wa Uhasibu na wachache wa manunuzi, hali hii huathiri kwa kiasi kikubwa katika tafsiri ya sheria za manunuzi hasa kwa ambao hawajasomea manunuzi, hapa nashauri CAG kuongeza idadi ya wakauguzi waliyosomea fani zamanunuzi ili kuweka usawa katika kufanya maamuzi ya hoja yanayohusu manunuzi ya Umma

e. PCCB, kuwa na mikakati ya kushiriki shughuli za kila siku kama sehemu ya utekelezaji wa sera yao ya kupambana na kuzuia rushwa. Hapa nitatoa mfano halisi kabisa (Ofisis ya PCCB Miaka ya 2015-2019) mkoa flan, kulikuwa na wimbi kubwa sana la watumishi waliyokuwa na tuhuma za kupokea au kutoa rushwa, na katika mapitio yetu, tulibaini kuwa pia baadhi ya watumishi waPCCB hawakuwa waadilifu na hivyo, sehemu kubwa ya watuhumiwa walikuwa hawana makosa. Baada ya hali kuzidi kuwa mbaya vilio na malalamiko kuwa vingi kwa mateso waliyokuwa wanapitia hasa kwa watumishi wa Halmshauri, Serikali iliamua kumbadilisha mkuu wa Taasis hiyo na kupeleka mwingine. Ndani ya miezi 3, hali ilibadilika kabisa na lile wimbi la watu kushtakiwa lilipungua kwa asilimia kubwa. Mkuu yule alianzisha mfumo ambao nilimpongeza saana, kuwa kila mradi uliokuwa unaanzishwa katka Halmashauri/Mkoa ulikuwa na jarada/File lake pale PCCB, na hivyo shughuli za kila siku za mradi huo zilikuwa zinarekodiwa ndani ya file husika, sehemu iliyoonekana kuwa na mapungufu, wahusika wa mradi waliitwa na kushauriwa kuboresha maeneo yaliyoonekana hayako sawa. Hadi ivi tunavyoongea Mkuu yule amefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hakika anapongezwa. Kiongozi kama huyo alipaswa kuwa mfano kwa wengine. (Wanaoishi mkoa huo watakuwa wanafahamu, hili)

2. Maamuzi ya Maafisa masuuli na viongozi wakuu (DED,WUKURUGENZI, RAS, MAKATIBU WAKUU)

Hili liko wazi, ingawa huwa tunawaona watumishi waliyofanya maamuzi kwa shinikizo la wakubwa huwa hawajitambui, ni seme tu, kila mtu anahitaji furaha eneo lake la kazi, mara nyingi, mgogoro kati ya Mwajiri na mwajiriwa huishia kwa Mwajiriwa kuumia zaidi ya Mwajiri. Hivyo kuwepo kwa vyombo hivi vya ufuatiliaji kwa karibu katikaHalmahsuri zetu/Wizara na Mashirika, itasaidia kuboresha utendaji kazi katika utumishi umma, na watumishi wa ngazi za chini watakuwa na namna bora ya ushauri au utendaji kazi pasipo mashinikizoi ya wakubwa.

Dr, M.L N. Sioni tatizo kama nchi tukaja na maboresho ya kina katika maeneo yanayoliingizia taifa mzigo mkubwa wa matumizi, mfano, Eneo la manunuzi, hapa nathubutu kusema huwa hatufanyi kwa uzito wake, tunarahisha sana. Tafadhari, timu yako ifanye analysis ya kina kwa kuchukua maoni ya watendaji na hata wakuu wa taasisi kutoa maoni yao juu ya nini kifanyike kwenye eneo la manunuzi. (Taratibu za ununuzi ni za ajabu sana, huwezi fananisha taratibu za ununuzi wa karatasi kuwa sawa na magari, computer na dawa) siku moja nilikuwa napitia nyaka flani za ununuzi taasis x, nilishangaa sana, na sikumlaumu Yule afisa sababu alifuata taratibu, ingawa nilimwambia jambolo alikiri kuwa angefanya tofauti, baadhi ya wakaguzi huwa si waelewa na hivyo angejiingiza kwenye mgogoro.

Serikali imekuwa ikiwatuhumu hawa watu wa manunuzi kuwa wanachelewesha kazi, wanaiba, na mambo mengine mengi, lakini kiuhalisia, sio rahisi afisa wa manunuzi kufanya ivo kwakuwa mchakato wa manunuzi unashirikisha. Nadhani kada ya manunuzi ndio kada namba moja inayochukiwa hapa.

Dr, nakuomba sana kwakuwaumeamua kwa moyo wa dhati kabisa kufanya marekebisho, basi naomba uhakikishe inazama deep kabisa, ili sehemu ya manunuzi iwe na tija katika serikali yetu.

Mara nyingi sheria na kanuni zetu, zinalenga kuwakomoa watumishi wanaozisimamia sheria na sio kuleta tija kwa wananchi, huwezi kumbana mtumishi huku katika kumbana huko kunasababisha huduma mbovu kwa wananchi kama kucheleweshwa kwa huduma,

3. Wakaguzi kuwa na muda wa kutosha katika kuandaa taarifa zao.

Hilini jambo muhimu sana kwa kuwa maamuzi baadhi hufanywa kwa kuwa na muda mfupi wa kutosha, lakini pia kama ulivyosema CAG aboreshewe ofisi yake kwa kuongeza bajeti pamoja na watumishi. Hali hii itapelekea kuboresha huduma za ukaguzi ambazo zinaweza kufanyika hata kwa hatua za mradi/miradi, kuliko kusubiri mradi kufanyika ndipo unakuja na taarifa ya ubadhirifu au viwango duni.

Nimeandika bila kufuata mtiririko, hoja na mpangilio malumu, hii ni kwa sababu za kimsing na usalama.

Asante
Nimekuelewa vizuri..

Mimi.sio Mwigulu na Wala siko hapa kumjibia ila miongoni mwa uliyopendekeza ndio serikali inataka ifanye hivyo..

Mfano kwenye taasisi ambazo kuna wakaguzi wa ndani huwa wanafuatilia utekelezaji wa mradi from scratch tena hawaishii kufanya ukaguzi bali kufanya monitoring pia..

Shida ilikuwa inakuja ni kwamba unaemkagua ndio anatakiwa akuwezeshe pia taarifa ya ukaguzi huwa inajadiliwa na hao maafisa masuuli huwataka wakaguzi kuondoa baadhi ya hoja..

Pendekezo la serikali Kwa sasa litaziba hiyo ombwe..Kuhusu wakaguzi wa Nje kuvizia nadhani ndio maana wameamua kuajiri watumishi wengin Ili wasisubirie mwisho wa mradi..

Na jambo la mwisho wakubwa wanazingua.sana hasa wakiwa na maslahi na mradi husika.
 
Kenya, baada ya kufanya mabadiliko ya Elimu yao ambayo imekuwa CBC kwa sasa(competency based curriculum), sasa Benki ya Dunia imeitambua Kenya Kuwa na elimu bora katika Bara​
Mleta mada akili huna sio kazi ya benki yeyote duniani kutambua kiwango cha elimu kuwa ipi bora .Hivi kwa akili yako unsiona hiyo ni kazi ya benki ? Hata kama akili huna?
 
Taratibu zilizopo ni za hovyo, ndio mana nimeegemea kwenye upotevu wa fedha katika ufuatiliaji.

Nimetoa mfano flan wa mradi wa 45 M.

unavyosema hizi taratibu, basi ni haki kwa watendaji kufanye yale yaliyoko kwenye taratibu, ikiwemo kulipana posho hata kwenye kazi ambazo hazifai kulipwa posho.
Hapana.

Inawezekana kabisa taratibu zilizopo huzielewi.

Ninachoweza kukubaliana nawe ni kama watu wanajifanya wanafuata taratibu kumbe wanatumia mwanya huo kuvuruga taratibu zenyewe.

Sikubaliani nawe kabisa kwamba taratibu zilizopo ni mbovu. Sema hazitimizwi ipasavyo.

Ninaelewa wazi kabisa katika nchi yetu tulivyo na tabia ya kulaumu tu kila kitu huku hatutimizi yale tunayoyalalamikia sisi wenyewe.

Kwa bahati nzuri nimesoma hadi hapo ulipoelezea udhaifu wa hao watu katika ngazi hizo. Hukueleza chochote kinachoonyesha kuwa taratibu zilizopo hazifanyi kazi, bali kinachoonekana ni kuvunja taratibu kwa wahusika, tena kwa maksudi kabisa!

Na mbaya zaidi hawawajibishwi na yeyeyote. Je, hili nalo utasema taratibu haziruhusu?

Andiko lako, 'at least,' hadi nilipokomea na kushindwa kuendelea kusoma, lina udhaifu. Umeliwasilisha kama una maslahi ndani ya hayo unayoyazungumzia na kuyapendekeza yafanyike.
 
Mleta mada akili huna sio kazi ya benki yeyote duniani kutambua kiwango cha elimu kuwa ipi bora .Hivi kwa akili yako unsiona hiyo ni kazi ya benki ? Hata kama akili huna?
Taratibu mkuu YEHODAYA, haya ni majadiliano tu, mkuu wangu, hakuna sababu ya kuitana majina.

Kenya wameweka mfumo mzuri sana wa elimu yao sasa hivi kama kweli watatimiza wanayonuia kuyapata katika elimu hiyo.
Benki hiyo inayosifu, ni wadau wakubwa katika elimu katika nchi mbalimbali, hata hapa kwetu. Umesahau wale mabinti wa Magufuli waliopata uja uzito; na ile hela, (ngapi vile? Najua kilikuwa ni kitita cha kutosha).

Kwenye mambo kama haya tuwe na subira mkuu, kwa sababu ni mambo muhimu sana katika nchi yetu.

Ninasubiri kusikia/kuona kazi za Profesa (nonsense)- Mkenda, kwa kazi atakayoifanya akiwa hapo. Nina matarajio mazuri naye, kama nilivyokuwa nayo na yule mama wa Kigoma, ambaye kwa kweli sijui kwa nini alivurunda kwenye wizara ile!
 
Mleta mada akili huna sio kazi ya benki yeyote duniani kutambua kiwango cha elimu kuwa ipi bora .Hivi kwa akili yako unsiona hiyo ni kazi ya benki ? Hata kama akili huna?
Nilisema humu, sasa ivi Afya ya akili imekuwa tatizo sugu! Unadharau Benki ya Dunia ambayo imekuwa ikitoa misaada lukuki ya Elimu hapa Tanzania??

Unatatizo la Afya ya Akili!
 
Taratibu mkuu YEHODAYA, haya ni majadiliano tu, mkuu wangu, hakuna sababu ya kuitana majina.

Kenya wameweka mfumo mzuri sana wa elimu yao sasa hivi kama kweli watatimiza wanayonuia kuyapata katika elimu hiyo.
Benki hiyo inayosifu, ni wadau wakubwa katika elimu katika nchi mbalimbali, hata hapa kwetu. Umesahau wale mabinti wa Magufuli waliopata uja uzito; na ile hela, (ngapi vile? Najua kilikuwa ni kitita cha kutosha).

Kwenye mambo kama haya tuwe na subira mkuu, kwa sababu ni mambo muhimu sana katika nchi yetu.

Ninasubiri kusikia/kuona kazi za Profesa (nonsense)- Mkenda, kwa kazi atakayoifanya akiwa hapo. Nina matarajio mazuri naye, kama nilivyokuwa nayo na yule mama wa Kigoma, ambaye kwa kweli sijui kwa nini alivurunda kwenye wizara ile!
Mkuu Kalamu, kama ningewasilisha hoja kulingana na mjadala flani tuliofanya, hakika ningefahamika kirahisi!

Hii nafaham kuna ambao wanajua A-Z ya hiki kilichoandikwa, ingawa ni kama nimechanganya changanya ujumbe, na tayari kuna wanao nihisi, wamenijia inbox.

Kuna jambo liko ndani ya mada, ndio core issue, na inawaumiza sana.

Asante
 
Watu wanawaza kuongeza mabasi we unazungumza mambo ya ufuatiliaji matumizi.
 
Hayo yote umeandika ya nini hapa bongo?

Mwigulu aache kulamba Asali Je aumize kichwa chake hapa?
Mkuu tunaandika kwakuwa nafsi zinatusuta sana, kuna mambo yanaendelea aisee, unabaki kuinamisha kichwa chini.
 
Mkuu Kalamu, kama ningewasilisha hoja kulingana na mjadala flani tuliofanya, hakika ningefahamika kirahisi!

Hii nafaham kuna ambao wanajua A-Z ya hiki kilichoandikwa, ingawa ni kama nimechanganya changanya ujumbe, na tayari kuna wanao nihisi, wamenijia inbox.

Kuna jambo liko ndani ya mada, ndio core issue, na inawaumiza sana.

Asante
Mimi siyo mtaalam wa mambo haya, lakini najua hakuna 'rocket science' katika mambo haya ya kumfanya asiyekuwa mtaalam kuyaelewa, akijitahidi kuyaelewa.

Haya unayozungumzia hapa, ni sehemu moja tu, katika mambo ya sehemu zingine serikalini yasiyofanyika kama yalivyolengwa. Ukiangalia, kila sehemu kuna upungufu na malalamiko katika utendaji.

Sasa basi, katika sehemu yenu hii ya matumizi ya fedha za waTanzania, kila mwaka, ndiyo nimesema kila mwaka karibu malalamiko ni yale yale; na hasa kila baada ya Mkaguzi Mkuu wa serikali anapowasilisha ripoti yake, kuna kelele nyingi sana husikika toka kila sehemu. Baada ya kelele hizo, kila kitu huwa kimya, kana kwamba hakuna chochote kilichotokea, na watu huendelea na shughuli zao kama kawaida, hadi msimu mwingine wa ripoti na kelele kupigwa!

Hivi kwa nini huwa hatujiulizi mambo yanakuwa hivi, na kuamua kuchukua hatua?

Watu na taasisi zote ulizozitaja humo kwenye andiko lako, wanarudia yale yale, mwaka hadi mwaka!

Sasa kama siyo ukichaa wa nchi yetu huu, sijui tuuite kitu gani!

Kila mara nasema humu, kwenye jukwaa hili hili la JF, kwamba wataalam sasa, nchi yetu haina uhaba nao katika nyanja mbalimbali; bali tatizo hawa wataalam hatujui kuwatumia, na mara nyingi tunawageuza kuwa ndio wanakuwa kikwazo kikubwa katika ufanisi wa nchi yetu.

Taratibu zipo, lakini hazifuatwi au zinageuzwa kuwa uchochoro wa kupitishia uchafu.

Nini Kifanyike kubadili hali?
Ngoja niache hili swali likielea. Lakini naamini bila wasiwasi kabisa kwamba inawezekana sana kukomesha upuuzi huu mwingi uliomo ndani ya serikali.
 
Ukifuatilia bajeti ya ufuatiliaji wa fedha za umma, hakika utalia mkuu!

Matumizi ni makubwa sana yanayoingia mifukoni mwa watu! sijui tatizo ni nini hasaa! Je mamlaka hazioni au ni makusudi??
Kiila mmoja anakula kwa urefu wa kamba yake..
 
Kiukweli, tunasafari ndefu sana, jambo hili ni kama masihara lakini usemacho ni kweli kabisa.
Bado Sana, uongozi ni ajira binafsi kwa maslai binafsi na sio wito wa kutumikia umma
 
Nchi masikin lkn imejawa milolongo miingi ya ufuatiriaji wa miradi, huu ni upumbavu.

Nchi masikin lkn imejawa ngazi nyingi za viongoz wasio na tija, binafsi huwa sioni umuhimu wa kuwa na wakurugenzi ktk wilaya kama kuna mkuu wa wilaya.

Binafsi sioni umuhimu wa mradi mdogo kufuatiliwa na rundo la viongoz, na bado mradi unakwama ama kuzingua.

As my wish kwa wenye nchi, Mfumuko wa muundo wa serikali ni muhimu sana kwa hii nchi, tunaweza kuwa tunazunguka sana kumbe tatizo ni sisi wenyewe,

Ondoa/futa kabisa baadhi ya levels za watumishi kama hao wakurugenzi, sjui madiwani, wenye viti wa mitaa, na hao waitwao mameya wa jiji maana hawana maana zaidi ya kuongeza upigaji.

Inauma lkn ndio ukweli, hiyo pesa inapotea kwa kuendekeza milolongo mingi ya ufujaji pesa wakat nchi yenyewe masikini.

Mabadiriko ni ngumu kutokea bila kumpata kiongozi sahihi, na tusije tegemea mabadiriko kutoka kwa hizo aina za wanasiasa wakina mwigulu&Sa[emoji817].

Hii nchi upigaji upo kwanzia ngazi ya mkuu wa nchi mpka kwa mtendaji wa mtaa, so kila mtu anapiga kwa nafasi yake.

Mabadiriko ni rahis sana kuyafikiria ukiwa nje ya system, lkn ukishaingizwa na kuanza kulambishwa asali ambayo ni jasho la watanzania, hakika unasahau mpaka majukumu yako ktk taifa.

Tuombe tu aje atokee kiongozi makini nje ya haya majambazi ya c+c+m
 
Mimi siyo mtaalam wa mambo haya, lakini najua hakuna 'rocket science' katika mambo haya ya kumfanya asiyekuwa mtaalam kuyaelewa, akijitahidi kuyaelewa.

Haya unayozungumzia hapa, ni sehemu moja tu, katika mambo ya sehemu zingine serikalini yasiyofanyika kama yalivyolengwa. Ukiangalia, kila sehemu kuna upungufu na malalamiko katika utendaji.

Sasa basi, katika sehemu yenu hii ya matumizi ya fedha za waTanzania, kila mwaka, ndiyo nimesema kila mwaka karibu malalamiko ni yale yale; na hasa kila baada ya Mkaguzi Mkuu wa serikali anapowasilisha ripoti yake, kuna kelele nyingi sana husikika toka kila sehemu. Baada ya kelele hizo, kila kitu huwa kimya, kana kwamba hakuna chochote kilichotokea, na watu huendelea na shughuli zao kama kawaida, hadi msimu mwingine wa ripoti na kelele kupigwa!

Hivi kwa nini huwa hatujiulizi mambo yanakuwa hivi, na kuamua kuchukua hatua?

Watu na taasisi zote ulizozitaja humo kwenye andiko lako, wanarudia yale yale, mwaka hadi mwaka!

Sasa kama siyo ukichaa wa nchi yetu huu, sijui tuuite kitu gani!

Kila mara nasema humu, kwenye jukwaa hili hili la JF, kwamba wataalam sasa, nchi yetu haina uhaba nao katika nyanja mbalimbali; bali tatizo hawa wataalam hatujui kuwatumia, na mara nyingi tunawageuza kuwa ndio wanakuwa kikwazo kikubwa katika ufanisi wa nchi yetu.

Taratibu zipo, lakini hazifuatwi au zinageuzwa kuwa uchochoro wa kupitishia uchafu.

Nini Kifanyike kubadili hali?
Ngoja niache hili swali likielea. Lakini naamini bila wasiwasi kabisa kwamba inawezekana sana kukomesha upuuzi huu mwingi uliomo ndani ya serikali.
Haya ni matokeo ya kufanya kazi kwa kuviziana ili kuonekana taasis flan inafanya kazi.

Kungekuwa na mfumo wa utendaji kazi wa pamoja, hayo yasingekuwepo.

Ndio mana nasema, tusione aibu kubadilisha mifumo yetu, hasa inayotusababishia gharama katika mipango ya miradi ya maendeleo
 
Nchi masikin lkn imejawa milolongo miingi ya ufuatiriaji wa miradi, huu ni upumbavu.

Nchi masikin lkn imejawa ngazi nyingi za viongoz wasio na tija, binafsi huwa sioni umuhimu wa kuwa na wakurugenzi ktk wilaya kama kuna mkuu wa wilaya.

Binafsi sioni umuhimu wa mradi mdogo kufuatiliwa na rundo la viongoz, na bado mradi unakwama ama kuzingua.

As my wish kwa wenye nchi, Mfumuko wa muundo wa serikali ni muhimu sana kwa hii nchi, tunaweza kuwa tunazunguka sana kumbe tatizo ni sisi wenyewe,

Ondoa/futa kabisa baadhi ya levels za watumishi kama hao wakurugenzi, sjui madiwani, wenye viti wa mitaa, na hao waitwao mameya wa jiji maana hawana maana zaidi ya kuongeza upigaji.

Inauma lkn ndio ukweli, hiyo pesa inapotea kwa kuendekeza milolongo mingi ya ufujaji pesa wakat nchi yenyewe masikini.

Mabadiriko ni ngumu kutokea bila kumpata kiongozi sahihi, na tusije tegemea mabadiriko kutoka kwa hizo aina za wanasiasa wakina mwigulu&Sa[emoji817].

Hii nchi upigaji upo kwanzia ngazi ya mkuu wa nchi mpka kwa mtendaji wa mtaa, so kila mtu anapiga kwa nafasi yake.

Mabadiriko ni rahis sana kuyafikiria ukiwa nje ya system, lkn ukishaingizwa na kuanza kulambishwa asali ambayo ni jasho la watanzania, hakika unasahau mpaka majukumu yako ktk taifa.

Tuombe tu aje atokee kiongozi makini nje ya haya majambazi ya c+c+m
Mkuu umeonge kwa uchungu sana, nikweli kabisa upigaji umekithiri , na sioni dalili za kujinasua hapa tulipo.

Kila mtu anamawazo ya upigaji tu! Mungu atusamehe kwakweli!
 
Nimeandika bila kufuata mtiririko, hoja na mpangilio malumu, hii ni kwa sababu za kimsing na usalama.
Mbona hatuna shida ya usalama wasiwasi wako wa nini Tena?
===
Asante kwa kutetea hoja zako vyema. Hasa hili la fedha nyingi kusimamia fedha kidogo! Mwisho wa siku mradi haukidhi thamani ya hela. Bila kubana na kudhibiti matumizi ya serikali kwa kujikita kuimarisha na kukamilisha miradi ya maendeleo, hata tukiwatoza kodi na tozo sisimizi wadudu wote wanaopatikana Tanzania kamwe hatutakuja kujitegemea kiuchumi.
 
Back
Top Bottom