Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekataza tabia ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka kuombwa fedha za mafuta ili kuwawahisha hospitalini kwa kutumia magari ya wagonjwa.
Akizungumza Septemba 14, 2026, wakati wa ziara mkoani Simiyu, wilayani Itilima, Dkt. Nchemba amesema sheria na miongozo ya huduma za afya haziagizi wagonjwa kulipia mafuta ya ambulensi, akibainisha kuwa kufanya hivyo ni uzembe wa watendaji.
Amewahimiza wananchi wanaouguza wagonjwa kutoa taarifa mara moja endapo watakutana na hali hiyo, ili wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu.