GE2025 Dkt. Mwigulu Nchemba aibuka kinara kwa kupata kura 10,604 - jimbo la Iramba Magharibi

GE2025 Dkt. Mwigulu Nchemba aibuka kinara kwa kupata kura 10,604 - jimbo la Iramba Magharibi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameongoza kwenye kura za maoni zilizopigwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Jimbo la Iramba Magharibi ambapo amepata kura 10,604

Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewapita kwa kura nyingi wapinzani wake watatu, ambao ni Ndugu Eng. Jumbe Naligia KATALA, Ndugu Emiliana Fanuel SAMSON, Ndugu Michael P. LEMMY ambapo alikuwa akichuana nao katika kinyang'anyiro hicho

Akizungumza mara baada ya kutangazwa matokeo hayo, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewashukuru sana wajumbe kwa kumpa kura za kishindo huku akiahidi kuwatumikia wananchi Jimboni endapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampitisha kuwania Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi

#KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki
#KaziIendelee

WhatsApp Image 2025-08-05 at 18.18.33.jpeg
 
Back
Top Bottom