Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkono kampeni ya kununua jezi halisi (original) za timu ya Simba SC, akitoa rai kwa wapenda soka wote kuepuka jezi bandia (feki).
Dkt. Mwigulu ameunga mkono kampeni ya kuhamasisha mashabiki kukataa jezi feki na kununua orijino kwa kununua jezi 200.
Amesema jezi feki zinaikosesha timu mapato muhimu kwa ajili ya usajili wa wachezaji bora, na pia zinaikosesha serikali mapato ya kodi.
Ameyasema hayo nyumbani kwake Misigiri Iramba Mkoani Singida, alipotembelewa na ugeni wa timu ya mauzo ya simba ukiongozwa na Msemaji wa Timu hiyo Ahmed Ally.
Yeye aweke mambo sawa kitaa ili watu tubakia na disposable income hizo jezi tutanunua tu (unadhani yale matozo kwenye simu waliyoweka tungekuwa na hizo chenji ni sawa na jezi ngapi ) !????
Maadui wetu hawajawahi Kubadilika Umasikini, Ujinga na Maradhi..., Vilevile Mahitahi Muhimu ya Binadamu hayabadilika (Chakula Malazi na Mavazi); Karne ya sasa ambayo sio kila mtu anaweza kuchukua Jembe na kwenda kulima mihogo na kupata kitoweo Pesa inahitajika. Hii ndio itakupatia mahitaji (ukizingatia hata zile huduma za elimu na afya zimekuwa biashara).
Hivyo tutakuwa hatumtakii mema mwananchi huyu hata kile ambacho hakitoshi bado tutakichukua kwa Matozo, na kama hio haitoshi zile huduma zote ambazo ni muhimu bado tukampa kwa gharama isiyo ya lazima.