Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa tasnia ya mazao ya bustani siyo tu sehemu ya sekta ya kilimo, bali ni sekta ya kimkakati ya biashara ya kimataifa inayounganisha Tanzania na Masoko ya Dunia.
Amesema kuwa kwa kutambua umuhimu huo, Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa ruzuku ya pembejeo iliyosaidia kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya bustani kutoka tani milioni 7. 5 kwa mwaka 2023/2024 hadi kufikia tani milioni 9. 7 kwa mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 30.2.
Amesema hayo (Jumatano, Aprili 22, 2026) alipozindua maandalizi kuelekea Jukwaa la Hotikacha la Kimataifa la Biashara na Uwekezaji (Hortilogistica Africa 2026) lenye lengo la kukuza biashara ya mazao ya bustani, hafla hiyo imefanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jukwaa la Kilimo wa Dkt. John Samwel Malecela Nzuguni jijini Dodoma. Jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika jijini Arusha, Novemba 08 hadi 10, Mwaka huu.