Dkt. Mwigulu: Tunapendekeza kuanzisha chombo cha usuluhishi wa masuala ya kikodi

Dkt. Mwigulu: Tunapendekeza kuanzisha chombo cha usuluhishi wa masuala ya kikodi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema watapendekeza kuanzisha chjombo cha msuluhishi wa masuala ya kikodi ili kuepuka kero zilizopo.

Mwigulu amesema hali ilivyo kwa sasa mtu akifanyiwa makadirio ya kodi na asipokubaliana nayo, analazimika kumfuata huyohuoyo aliyemkadiria kuongea naye, ambapo pia huwa anatakiwa kutoa theluthi moja ya makadirio.

Ametoa mfano wa mianya ya rushwa iliyopo katika mfumo huo ambapo watumishi huomba fedha ili kuwapunguzia makadirio ya kodi watu wanaolalamikia malalamiko.
 
Hawa wapuuzi wanatuongezea mzigo walipa kodi, tuanze kulipa mishahara na posho watu wengine ambao hawana kazi yoyote
 
cha kwanza, ni kupunguza kodi kubwa zisizo na tija na zenye kero.

VAT at least ifike 16% kama kenya, kama siyo kuishusha kabisa hadi single digit.

kwann kuwepo na ukadiriaji?
Kodi itozwe kwa kanuni maalumu..

Mwisho, ni serikali yenyewe ndiyo inafuja kodi kwa matumizi yasiyo na maana, mfano ununuzi wa V8. Hizo gari ni aghali ni za anasa, nanuendeshaji wake ni aghali..
 
Nchi imejaa idara nyingi ambazo hazina ufanisi wowote
Wapishi wengi huishia kuharibu mchuzi. Nilisikia JPM akisema, ^Imefikia hatua kwenye nchi yetu kamati inakaa kuunda kamati itakayokwenda kuchunguza tuhuma za kamati iliyochaguliwa ili kuchunguza ubadhirifu wa fedha uliofanywa na kamati fulani iliyopewa dhamani ya kuwahudumia wananchi.^

Kiwango hiki cha ujinga ndicho kinamfanya Elon Musk na SpaceX yake afanye jitihada day in and day out kuhamia Planet Mars.
 
Sawa
 
Kwani chombo Cha Rufani ya Kodi na hiki tofauti yake Nini? Maana wao pia wanafanya kazi hizi hizi..Huu nimrundikano wa tume.wangeboresha kile kile Cha Rufani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Naomba kuuliza, hiki ni kitu gani au nchemba anatuona mafala?

Registrar,

Tax Revenue Appeals Tribunal

Ex-BIT Building

2nd Floor,

Samora Avenue

P.O. Box 9721

Dar es Salaam

Tanzania

Tel: 022 213 4557 / 022 213 4558

Email:registrar@trat.go.tz

:barua@trat.go.tz

Website: www.trat.go.tz

1624357241570.png
We have now moved to Hazina offices, Madaraka Street 1stFloor
 
Tax ombudsman kwa mazingira ya Tanzania umakini inahitajika kabla ya yote.
 
Back
Top Bottom