Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Suala zima la migomo Kariakoo linahusu masuala mazima ya kodi, liliibuka mwaka jana likazimwa kisiasa likaibuka tena mwaka huu na linazimwa kwa mbinu zile zile za kisiasa.
Linaacha ukakasi kwa wote wenye kutafakari kila suala kwa kina. Linakuja na kuondoka likiwa na haki kabisa ya kumuondoa Waziri Mwigulu Nchemba pale wizara ya fedha. Mamlaka za uteuzi zinajifanya hazisikii kuhusu uhalali wa kilio cha haki kabisa cha nafasi ya Mwigulu.
Mheshimiwa Mwigulu kwanza ni jeuri sana na mwenye kusahau kuwa binadamu kwa sifa yake ni mpita njia tu juu ya uso wa dunia. Hana kabisa chembe chembe za unyenyekevu katika wasifu wake mzima. Pili, hafahamu kwamba yanayofanyika sasa hivi chini yake kuna siku yatakuja kuwekwa hadharani na yatakuja kuwa sehemu ya habari za ukurasa wa kwanza ambazo zinaendelea ukurasa wa tatu na wa nne. Ukifika muda huo huu ubora anaodhani anao utabadilishwa na sura ya kinafiki iliyojaa unyonge kila atakapopeana mkono na mtu fulani.
Mwana CCM mwenzake January Makamba anayo pia sifa mbaya ya 'upigaji' lakini angalau yeye anafahamu sana namna ya kuishi na watu na kujishusha pale anapotakiwa ajishushe, anakubalika miongoni mwa wastaarabu kwa hulka yake hiyo ya kufahamu kujichanganya na kujinyenyekeza.
Maisha haya ni sawa na upepo wa baharini wenye kupita kwa kasi na haurudi tena kule ulipotoka. Haya magari ya msafara wake na ufahari wote wa cheo chake huku akilindwa na mamlaka ya uteuzi kuna siku kila kitu kitaongelewa kwa sentensi za muda uliopita. Anaotunishiana nao misuli watakuwa wakimuongelea kwa kejeli wakati huo ukifika na hawatakuwa na msaada kwa mustakabali wake.
Mawaziri wa awamu ya sita kumbukeni kujishusha katika kila mnachokifanya. Ukiweza kuiishi unyenyekevu haulazimiki kutumia nguvu kubwa katika siku ambazo MFALME ni mwingine.
Hautalazimika kujikomba sana na kujifanya upo karibu na utawala mpya ikiwa uliishi vizuri na kila mtu wakati mkate wake ukiwa umepakwa siagi ya kutosha.
Ulitaka kuwa Rais wa awamu ya tano, Mungu hakuwataka wewe pamoja na wengine wengi wa rika lako. Hizi hulka zote unazozionyesha muda huu ni ushahidi wa urais wako ungekuwa vipi iwapo ungepitishwa na CCM kuwa mgombea urais.