Dkt. Mwigulu: Waunganishieni umeme wananchi kwa Shilingi 27, 000

Dkt. Mwigulu: Waunganishieni umeme wananchi kwa Shilingi 27, 000

Mchawi ni January Makamba na wizi wake, aliikuta wizara iko vizuri kabisa chini ya mbunge wa Chato Dr Kalemani kufika yeye tu na liupara lake akaanza mazingaombwe ya miradi ya upigaji na kufuta bei ya 27,000/=
 
Kwa hiyo kafuta kauli ya Bi Kizimkazi kuwa hakuna wa 27K?
Mbona nchi hii ina mambo ya ajabu ajabu? Ndio maana wawekezaji genuine woote hawaji
hajafuta hiyo kauli, ukifatilia issue ya kuunganishwa umeme kwa 27K. kuna mambo mawili

1. Uhalisia wa mambo ni kwamba Tanesco haiwezi kufanya jambo hilo maeneo yote, shirika linahitaji hela kwa sababu serikali inawataka watengeneze faida, hivyo hiyo 27K wanaitekeleza sana vijijini, na eneo likionesha uchangamfu hawafanyi kwa 27K

2. Upande wa pili viongozi wanaongea tu hiyo kauli ila hata wao wanajua jambo haliwezekani kufanywa nchi nzima, ila wanaonge ahivyo kutuliza wananchi.
ukiachana na Mwigulu, hata MAkamu wa Rais Ndejembi naye kasema jambo kama hilo na hata habari za taneso kukopesha unit, ila anasema hivyo baada ya yeye kutoka kua waziri wa Nishati - hakufanya hayo anayoyasema
 
Ooh kumbe Magufuli was right, mbona mama alikuja akakanusha kwamba it's impossible kuunganishwa kwa 27k, nini kimetokea hadi leo 27k itoshe.

Hawa watawala wamekuwa watu wa ajabu sana.
 
Mchawi ni January Makamba na wizi wake, aliikuta wizara iko vizuri kabisa chini ya mbunge wa Chato Dr Kalemani kufika yeye tu na liupara lake akaanza mazingaombwe ya miradi ya upigaji na kufuta bei ya 27,000/=
mbona hata yeye kalemani alikua anatekeleza jambo hilo kwa kusuasua?
 
Ooh kumbe Magufuli was right, mbona mama alikuja akakanusha kwamba it's impossible kuunganishwa kwa 27k, nini kimetokea hadi leo 27k itoshe.

Hawa watawala wamekuwa watu wa ajabu sana.
Siasa hizo ndugu ....

Angalau ndio mbinu ya kurejesha ushawishi kwa Umma uwaamini baada ya kile walichokitenda mwaka Jana
 
Waache upumbavu, Wapitishe sheria mambo yawe kwenye maandishi, sio matamko tu ya kwenye mikutano.
Mhh si kuna clip ikionesha kwamba uanganishwaji umeme kwa bei hiyo haiwezekani kabisa, tulipotoshwa na sasa timejilidhisha huwezi kabisa unganishwa umeme kwa 27k.
Habari, ndugu mteja.

Bei ya kuunganishwa umeme kwa 27,000/- inaruzuku ndani yake ya kuleta unafuu kwa wateja wa vijijni.

Asante. ^MY
 
Habari, ndugu mteja.

Bei ya kuunganishwa umeme kwa 27,000/- inaruzuku ndani yake ya kuleta unafuu kwa wateja wa vijijni.

Asante. ^MY
Kauli ya Waziri Mkuu ni ya jumla akimaanisha wateja wote wanaohitaji umeme wanapaswa kulipia Tsh.27,000/= tu na si vinginevyo

Tafadhalini wekeni taarifa kwa umma kufafanua kauli yake kila mmoja aelewe
 
Kauli ya Waziri Mkuu ni ya jumla akimaanisha wateja wote wanaohitaji umeme wanapaswa kulipia Tsh.27,000/= tu na si vinginevyo

Tafadhalini wekeni taarifa kwa umma kufafanua kauli yake kila mmoja aelewe
hapa aliyepuyanga ni PM aidha kwa kujua au bila kujua
 
𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗪𝗜𝗚𝗨𝗟𝗨 - 𝗪𝗔𝗨𝗡𝗚𝗔𝗡𝗜𝗦𝗛𝗜𝗘𝗡𝗜 𝗨𝗠𝗘𝗠𝗘 𝗪𝗔𝗡𝗔𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗜𝗟𝗜𝗡𝗚𝗜 𝟮𝟳,𝟬𝟬𝟬

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendelea kuwaunganishia umeme wananchi kwa gharama ya Shilingi 27,000

Ametoa agizo hilo Oktoba 16, 2026, alipokuwa akizungumza na wananchi mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja.
Habari,

Asante kwa taarifa, taasisi yoyote ya serikali inaongozwa kwa sheria, kanuni,taratibu na miongozo.

Hivyo maelekezo ya Waziri Mkuu ni halali, kazi yetu Kama wataalam ni kutekeleza.

Asante. ^MY
 
Back
Top Bottom