GE2025 Dkt. Mwinyi aahidi kuongeza barabara na skuli za ghorofa pangawe - Zanzibar

GE2025 Dkt. Mwinyi aahidi kuongeza barabara na skuli za ghorofa pangawe - Zanzibar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kuimarisha miundombinu ya barabara na sekta ya elimu ili kuleta maendeleo makubwa Unguja na Pemba.

Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Pangawe, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dkt. Mwinyi amesema serikali atakayoiongoza itaongeza mtandao wa barabara za kisasa katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ili kurahisisha usafiri na biashara za wananchi.

Soma > Dkt. Mwinyi azindua huduma ya Water Taxi Zanzibar

Aidha, ameahidi kuendelea na ujenzi wa skuli za ghorofa, hatua itakayosaidia kuondoa changamoto ya wanafunzi kusoma kwa zamu mbili – asubuhi na jioni – na badala yake kupata fursa ya kusoma kwa mazingira bora na wakati sahihi.

Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa dhamira yake ni kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua kubwa za kimaendeleo, akibainisha kuwa sera za CCM zinagusa maisha ya kila mwananchi kupitia miradi ya elimu, miundombinu, huduma za jamii na uchumi.

“Tunataka Zanzibar yenye maendeleo makubwa Unguja na Pemba ambapo kila mwananchi atafaidika na fursa za kijamii na kiuchumi,”

Wananchi wa Pangawe walimpongeza kwa ahadi hizo na kueleza matumaini makubwa kwamba utekelezaji wake utaleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yao ya kila siku.

 
Back
Top Bottom