Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi afunga kampeni Zanzibar

Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi afunga kampeni Zanzibar

CCM Damu

Member
Joined
Oct 29, 2007
Posts
15
Reaction score
28
Mgombea wa Urais Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa dhamira yake ya kuwatumikia Wazanzibari iko imara tofauti na wakati mwingine huku akieleza kuwa kampeni za Urais zimemuwezesha kujua uzito wa dhamana ya nafasi hiyo anayoiomba.

Akizungumza na umati wa watu waliojitokeza katika mkutano wa kufunga kampeni zake katika uwanja wa Demokrasia (Kibandamaiti) Dkt.Mwinyi ametaja idadi ya mikutano ya hadhara na isiyo ya hadhara aliyoifanya kuwa ni 75 visiwani humo.

“Ninaposimama kuomba kura ninasimama nikiwa na uelewa wa uhakika wa haja zenu, matamanio yenu na matumaini yenu halikadhalika kampeni hizi zimeniwezesha kutambua uzito wa dhamana wajibu unaoambatana na dhamana ya Urais ninaouomba" amesema Dkt. Mwinyi.

“Kuzunguka huku kumenipa fursa yakutafakari nakujipima tena na tena nimeridhika kuwa dhamira yangu yakuwatumikia wazanzibari iko imara sasa kuliko wakati mwingine wowote” ameongeza Dkt. Mwinyi

Dkt. Mwinyi amefunga kampeni zake visiwani humo huku akisindikizwa na baadhi ya viongozi akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, Samia Suluhu mgombea mwenza wa Urais Tanzania bara sambamba na Rais Dkt. Ali Shein anayemaliza muda wake Zanzibar.

B5FDEAC7-68BB-4007-A257-F5E99D0710B0.jpeg
CEEEA0B5-2B03-4A17-A4C5-55B78B93C7DB.jpeg
979008A9-4B40-4191-896A-1D19E33F8C30.jpeg
DE4DC251-81B4-4B50-842A-7B0D60FCE4DB.jpeg
F9E40886-6F48-462D-815F-AE90D608C53D.jpeg
3B118D95-B4F5-45D7-B9CF-76B71D82C383.jpeg
662B90BD-6EFC-4EE0-B5F0-D67F6E9BB6C5.jpeg
 
Kura zitakazo pigwa tarehe mbili tofauti kwa nchi ambayo tangu kampeni kuanza ni mikutano 75 tu ndio imefanyika.

Ni maajabu.
 
Jamani tar 28 tusifanye mchezo agenda ni kumchagua Mwinyi tu huyo babu akatafute shughuli nyengine ya kufanya.
 
Namuonea huruma sana Hussen Mwinyi kutamani mfupa zama hizi. Huenda yeye na familia yake wakose uhuru hata wa kuchangamana.
JK zama zile serikali umoja wa kitaifa angewejeza B 50 pekee,kwa kina Maalimu Seif kisha kura ya maoni tukawa nchi moja.
 
ukiangalia picha zote nane unaona jamaa wamekubali kushindwa

Maalim ndiye wa kumaliza mchezo...awe ngangari
 
Hizi siku zikizobaki hakuna kulala,kila mtu awe mlinzi wa mwenzake,kuepuka lawama za kuibiwa kura
 
Nimemsikiliza Dr Mwinyi anafaa kuwa Rais,hana ubaguzi,na anajua kuwa wananchi wanataka nini?
 
Rais wa awamu ya sita (6) anayesubiri kuapishwa
Mgombea wa Urais Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa dhamira yake ya kuwatumikia Wazanzibari iko imara tofauti na wakati mwingine huku akieleza kuwa kampeni za Urais zimemuwezesha kujua uzito wa dhamana ya nafasi hiyo anayoiomba...
 
Back
Top Bottom