PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema endapo akipata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar kwa miaka mitano ijayo atahakikisha anavuka lengo la utoaji wa ajira 300,000.
Kauli hiyo ameitoa wakati akihutubia wananchi wa Bumbwini kwenye uwanja wa Bumbwini Kidmini uliopo wilaya ya Kaskazini B mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Tunavyozungumza kuna mkopo mmoja wa kilimo na wafugaji ambao utachukua vijana wengi sana mradi huu unathamani ya dola milion 180 leo nimepata taarifa umekubalika hivyo vijana wengi watajiajiri wenyewe,”amesema
Amesema ahaadi yake kama alivyofanya kwenye eneo la elimu, afya na barabara safari ya miaka mitano ijayo atafanya kwa upande wa utoaji wa ajira kwa vijana.
Dkt. Mwinyi amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita aliahaidi ajira 300,000 na kwamba mpaka sasa ajira 217,500 zimetolewa ikiwa sawa na asilimia 72.5 na kwamba awamu ijayo atavuka lengo hilo.