PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali itaangalia uwezekano wa kujenga gati au kuchimba sehemu maalum ya bandari katika Kisiwa cha Kojani ili kurahisisha huduma ya boti ya wagonjwa kufanya kazi saa 24 bila vikwazo.
Akizungumza na wananchi wa kisiwa hicho mara baada ya kukabidhi boti ya ambulance, Dkt. Mwinyi amesema serikali imejipanga kuboresha huduma za afya na elimu, ikiwemo ujenzi wa skuli mpya za ghorofa na kituo cha afya cha kisasa kinachohudumia zaidi ya watu 9,000.
Amesema, serikali itaendelea kuinua maisha ya wananchi wa visiwani kwa miradi ya maendeleo, mikopo ya vijana na wanawake, pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafiri wa baharini.
Wananchi wa Kojani wamemshukuru Dkt. Mwinyi kwa juhudi zake na kumuombea ushindi katika uchaguzi ujao ili aendelee kuwatumikia kwa miaka mitano mingine.