Dkt. Mwinyi ateua Mawaziri wanne kutoka ACT Wazalendo

Dkt. Mwinyi ateua Mawaziri wanne kutoka ACT Wazalendo

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
23,234
Reaction score
28,473
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza uteuzi na uhamisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri, pamoja na mabadiliko ya miundo ya baadhi ya wizara, ikiwa ni sehemu ya kukamilisha uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa kuwajumuisha mawaziri kutoka ACT-Wazalendo.

Rais Mwinyi ametangaza mabadiliko hayo leo, Oktoba 3, 2026, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu Zanzibar.

Katika mabadiliko hayo, ACT-Wazalendo imepata nafasi nne za uwaziri. Nassor Ahmed Mazrui ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya; Omar Said Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda; Dkt. Nasra Nassor Omar, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale; na Dkt. Mohamed Ali Suleiman, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametangaza mabadiliko ya miundo ya baadhi ya Wizara, ikiwemo kuhamishia masuala ya Mipango Ofisi ya Rais, Ikulu, na kuanzishwa kwa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.

Mabadiliko mengine ni pamoja na Shaaban Ali Othman kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Mipango na Usimamizi wa Utendaji Serikalini; Masoud Ali Mohamed, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Uhusiano wa Jamii; Mudrik Ramadhan Soraga, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi; na Ali Suleiman Ameir Mrembo, Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.

Rais Dkt. Mwinyi amesema mabadiliko hayo yanaendelea kutekeleza makubaliano ya maridhiano baina ya CCM na ACT-Wazalendo kuhusu uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Mawaziri na Naibu Mawaziri wote walioteuliwa na waliohamishwa wataapishwa Jumatatu, Oktoba 5, 2026, saa

Likitokea hili bara,nani atafaa hata kwa uwaziri?--hakuna!.
8:00 mchana.
1000017566.jpg
 
ACT imeshajifia. Huwa nashangaa inakuwaje OMO anatoka tu serikalini ana muovertake Jussa na Mazuri.
 
Back
Top Bottom